Ruiru
| Ruiru | |
| Nchi | Kenya |
|---|---|
| Mkoa | Kati |
| Wilaya | Thika |
Ruiru[1] ni mji katika Wilaya ya Thika, ipatikanayo katika Mkoa wa Kati nchini Kenya.
Yaliyomo |
Jiografia [hariri]
Mji huu uko katika umbali wa takribani kilomita 3 kutoka katika Mpaka wa Nairobi. unachukua ukubwa wa 292 km2 na umezungukwa na mashamba ya Kahawa. Ruiru ni moja kati ya miji inayotambulika zaidi nchini Kenya, ambao unaweza kufikika kwa urahisi kupitia barabara au reli.
Idadi ya Wakazi [hariri]
Mnamo 1999, Ruiru ilikuwa na watu takribani 100,000. Hata hivyo, mji huu umekuwa na ongezeko la idadi ya watu, kutokana na uhaba wa nyumba Mjini Nairobi. Idadi ya watu mjini humo ilikadiriwa kuwa 220,000[2] Mji huu umeng'ang'ana kuwatosheleza wakazi wake.
Uchumi [hariri]
Wengi wa Wakazi wa Ruiru ni wanabiashara wa asili ya Kikuyu. Mji huu pia una matawi ya benki mashughuli kama vile Benki ya Equity, Benki ya Family, Benki ya Cooperative na Benki ya Barclays Pia kuna viwanda mbalimbali katika mji huo.
Tazama Pia [hariri]
Wilaya ya Thika Mkoa wa Kati Barabara kuu ya Thika-Nairobi
Viungo vya Nje [hariri]
Virejeleo [hariri]
- ↑ Ukuaji wa Maeneo, Metropolitan Nairobi www.earth.columbia.edu
- ↑ Ruiru, Kenya: [1].
Anwani ya kijiografia: 1°08′56″S 36°57′25″E / 1.14889°S 36.95694°E
| Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ruiru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
