Kajiado

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Kajiado


Kajiado
Kajiado is located in Kenya
Kajiado
Kajiado

Mahali pa mji wa Kajiado katika Kenya

Majiranukta: 1°51′0″S 36°47′0″E / 1.85000°S 36.78333°E / -1.85000; 36.78333
Nchi Kenya
Kaunti Kajiado
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 18,281

Kajiado ni mji wa Kenya katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Mji wa Kajiado ni makao makuu ya Kaunti ya Kajiado.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya watu wanaoishi Kajiado ni 18,281 (sensa ya 2009) [1] Archived 1 Machi 2020 at the Wayback Machine.. Idadi kubwa ya watu wanaoishi Kajiado ni Wamasai.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina la Kajiado linatokana na neno "Orkejuado" ambalo linamaanisha "mto mrefu" katika lugha ya Kimasai. Mto huu upo magharibi mwa mji huu.

Jina halisi wa mji huu ni "Olopurupurana", ambalo lina maana ya "kilima cha mviringo".

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Mji huu upo kusini kwa jiji la Nairobi katika barabara kuu Nairobi - Arusha.

Mji wa Kajiado una kituo katika reli ya Magadi Soda Railway ambaye inatokea Konza mpaka Magadi.

Pia kuna vituo vya matatu za kwenda Namanga na Nairobi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]