Bungoma
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Bungoma | |
| Mahali pa mji wa Bungoma katika Kenya | |
| Anwani ya kijiografia: 0°34′0″N 34°34′0″E / 0.56667°N 34.56667°E | |
| Nchi | Kenya |
|---|---|
| Mkoa | Magharibi |
| Wilaya | Bungoma |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 60,650 |
Bungoma ni mji mdogo katika Kenya ya magharibi karibu na mpaka wa Uganda ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Bungoma. Kuna wakazi 60,000.[1] Bungoma iko kwa kimo cha mita 1,385 juu ya UB mguuni wa Mlima Elgon.
Wenyeji wa Bungoma ni Wabukusu ambao ni kitengo cha Waluhya.
Mji wa Bungoma ulianzishwa kama kituo cha reli ya Uganda katika miaka ya 1920. Bungoma ikateuliwa kama kituo cha mwisho ndani ya Kenya kabla ya kufikia mpaka wa Uganda. Wakati wa uhuru Bungoma ilionekana kama kijiji kikubwa chenye maduka machache. Mji ukaendelea kukua haraka.
Uchumi umetegemea hasa kilimo kinachostawi vizuri kutokana na hali ya hewa na uwingi wa mvua. Kuna kiwanda cha sukari. Kiwanda cha karatasi cha Webuye kipo karibu.
Marejeo [hariri]
- ↑ Kenya National Bureau of Statistics: Population of local authorities
| Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bungoma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |