Kericho
| Kericho | |
| Mahali pa mji wa Kericho katika Kenya | |
| Anwani ya kijiografia: 0°22′S 35°18′E / 0.367°S 35.3°E | |
| Nchi | Kenya |
|---|---|
| Mkoa | Bonde la Ufa |
| Wilaya | Kericho |
| Idadi ya wakazi (1999) | |
| - Mji | 85,000 |
Kericho ni mji wa Kenya ya kusini magharibi na makao makuu ya wilaya ya Kericho katika mkoa wa Bonde la Ufa mwenye wakazi 30,000 ambao pamoja na vitongoji wa nje hufikia 85,000 kwa eneo kubwa la mji.
Kiwango cha Kericho kutoka usawa wa bahari ni mita 2070. Ni kitovu cha eneo la mashamba ya chai. Makampuni makubwa ya chai yana ofisi mjini. Chai inayokuzwa Kericho ni mashuhuru kwa ladha yake nzuri na rangi ya kuvutia. Pia wilaya hii ina wanariadha wa kukimbia mbio za mbali wa hali ya juu sana ambao mara kwa mara wanashinda medali za dhahabu katika mashindano mbalimbali.
Kyanzo kya maji cha msitu mau ambacho ni kikubwa kuliko zote nchini Kenya kinapatikana mjini Kericho. Mji huu ni makao makuu ya sekta kubwa ya kilimo cha chai nchini Kenya. Makampuni makubwa ya chai kwa mfano Unilever Kenya' James Finlay na Williamson tea zinapatikana hapa. Chai inayokuzwa hapa huwa inasafirishwa na kuuzwa nchi za Uropa hasa Uingereza. Idadi ya wakazi wanaoishi mji huu ni 150,000 na idadi ya watu wote kwenye wilaya hii ni 500,000 (sensa 1999).
Historia na Utamaduni [hariri]
Eneo la mji hukaliwa kiasili ya Wakipsigis ambao ni sehemu ya Wakalenjin. Jamii ya wakipsigis wanasifika kuwa watu walioshika mila zao na pia watu wakarimu. Wanariadha wengi mashuhuri kwa mfano Kipchoge Keino wametoka katika jamii hii.
Chakula mashuhuri cha jamii hii ni kimyet(Ugali) ambayo inaliwa pamoja na mboga za majani, mursik(maziwa ya mgando) na nyama. Chai pia inanywewa sana katika jamii hii, hasa asubuhi na baada ya kula.
Jina la mjii huu linasemekana kwamba linatokana na mganga wa zamani wa kikipsigis aliyeitwa Kipkerich.
Usafiri [hariri]
Usafiri unaotumiwa sana ni wa magari. Barabara za wilaya hii zipo katika hali nzuri ukilinganisha na wilaya zingine nyingi za nchini Kenya. Barabara kuu tatu zinaelekea mjini Kericho, barabara ya Kisumu-Kericho, barabara ya Kisii-Kericho na barabara ya Nakuru-Kericho. Mabasi na matatu yanatumiwa kwenda miji mingine.