Kilifi
| Kilifi | |
| Mahali pa mji wa Kilifi katika Kenya | |
| Anwani ya kijiografia: 3°38′0″S 39°51′0″E / 3.63333°S 39.85°E | |
| Nchi | Kenya |
|---|---|
| Mkoa | Pwani |
| Wilaya | Kilifi |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 30,994 |
Kilifi ni mji kwenye pwani la Kenya uliopo kati ya Mombasa na Malindi. Iko kando la kihori cha Kilifi ("Kilifi Creek") kinachoishia katika Bahari Hindi. Mji ni makao makuu ya wilaya ya Kilifi katika Mkoa wa Pwani (Kenya).
Wakati wa sensa ya 1999 Kilifi ilikuwa na wakazi 30.994 [1].
Kilifi imekuwa kitovu cha utalii kimojawapo nchini Kenya hasa kutokana na fuko zake za kupendeza na Bofa Beach ni marufuku hasa. Mdomo mpana wa kihori unapendwa na wenye jahazi za burudani kuna jahazi nyingi zinazolala hapa.
Maghofu ya kihistoria ya Mnarani yako kando la mji wa Kilifi. Mabaki yanayoonekana ni misikiti mbili pamoja na makaburi yaliyokuwa sehemu ya mji wa Waswahili uliokuwa kituo cha biashara. Msikiti mkubwa ulianzishwa mnamo mwaka 1425; mji uliangamizwa wakati wa mashambulio ya Wagalla katika karne ya 17.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kilifi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |