Kisumu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kisumu ni mji mkuu wa Mkoa wa Nyanza nchini Kenya mwenye wakazi 322,724 (1999). Ni mku mkubwa wa tatu wa Kenya pia mji mkubwa wa Kenya ya Magharibi na makao makuu ya wilaya ya Kisumu.
Mji uko kando la ziwa Viktoria Nyanza una bandari kubwa ya nchi kwa ziwa hilo. Mji na bandari vilianzishwa kwa jina la "Port Florence" mwaka 1901 wakati reli ya Uganda ilipofika hapa kutoka Mombasa.
Kuna feri ziwani kutoka Kisumu kwenda Mwanza, Bukoba, Entebbe, Port Bell na Jinja.
Kiuchumi Kisumu ina viwanda kadhaa hasa za sukari, samaki na vitambaa pia ya bia.
Maendeleo ya Kisumu yalikwama miaka mingi kwa sababu Waluo walisimama upande wa upinzani wa kisiasa kwa miaka mingi na serikali haikupeleka miradi tena katika mkoa huu.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kisumu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |