Victoria (ziwa)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Viktoria Nyanza)
| Ziwa la Viktoria Nyanza | |
|---|---|
|
|
|
| Mahali | Afrika ya Mashariki |
| Nchi zinazopakana | Tanzania, Kenya na Uganda |
| Eneo la maji | 68,100 km² |
| Kina ya chini | 81 m |
| Mito inayoingia | Kagera, Katonga, Nzoia |
| Mito inayotoka | Nile |
| Kimo cha uwiano wa maji juu ya UB | 1,134 m |
| Miji mikubwa ufukoni | Kampala, Kisumu, Mwanza |
Ziwa Victoria (pia: Viktoria Nyanza, Ziwa Nyanza) ni ziwa kubwa Afrika, pia ni chanzo cha mto Nile, hili ni ziwa la pili kwa ukubwa Duniani. Ziwa la kwanza ni Ziwa Superior ambalo lipo Amerika ya Kaskazini. Ziwa Victoria lipo futi 3,726 kutoka usawa wa bahari na lina eneo la maili za mraba zaidi ya 26,000. Maji ya ziwa Victoria yanamiminika kwenye mto Nile na kuelekea bahari ya Mediteranea kwa umbali wa maili 4,000. Ziwa Victoria limekuwa ni kiunganisho na mpaka kwa nchi tatu za Afrika ya mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.
[hariri] Viungo vya Nje
Watersheds of Africa: A10 Nile | Lake Victoria
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Victoria (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |