Entebbe
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Entebbe katika Uganda.
Entebbe ni mji wa Uganda mwenye wakazi 90,000 uliowahi kuwa mji mkuu wa nchi. Iko kwenye mwambao wa Ziwa Victoria karibu na mji mkuu Kampala.
Jina la mji lamaanisha "kiti" kwa Kiganda kwa sababu hapa palikuwa mahali ambako chifu aliketi akisikia malalamiko ya watu na kuamua kesi.
1893 Entebbe ilikuwa makao makuu ya Waingereza walipoanza kujenga utawala wao katika Uganda. Entebbe iliendelea kama mji mkuu hadi 1962. Hadi leo kuna wizara kadhaa.
Entebbe kuna bustani ya wanyama ya kitaifa pia bustani ya utafiti wa mimea pamoja na taasisi mbalimbali kama vile taasisi ya utafiti wa virasi.
Mji umejulikana kimataifa kwa sababu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa uko Entebbe unaohudumia mji mkuu.