Samaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Samaki
Tengesi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Faila ya chini: Gnathostomata (Wanyama wenya mataya)
Ngeli: Cephalaspidomorphi (Mikunga wanyonyaji)

Chondrichthyes (Samaki wenye gegedu)
Actinopterygii (Samaki wenye mapezi yenye mihimili)
Sarcopterygii (Samaki wenye mapezi ya nyama)

Papa buluu

Samaki ni wanyama wenye damu baridi wanaoshi kwenye maji ya mito, mabwawa, maziwa au bahari. Wote ni vertebrata yaani huwa na uti wa mgongo. Wanatumia oksijeni iliyopo ndani ya maji kwa kuvuta maji kwenye mashavu yao.

Kuna aina nyingi za samaki wadogo wenye urefu wa sentimita moja na wakubwa wenye urefu hadi mita 15. Ila tu viumbe vikubwa kwenye maji si samaki bali nyangumi ambao ni mamalia.

Samaki na watu[hariri | hariri chanzo]

Tangu zamani samaki walivuliwa na watu. Samaki ni chakula bora kwa sababu nyama yake ina protini nyingi inayopokelewa kirahisi na mwili wa binadamu. Watu wanaoishi karibu na bahari au mito mikubwa mara nyingi ni wavuwi. Leo hii ni zaidi ya watu bilioni moja wanaotegemea samaki hasa kama chanzo cha protini.

Bali na kuvua tu watu wanafuga samaki pia. Ufugaji samaki hutokea hasa katika mwbwawa wadogo; samaki wanapewa lishe mle na baada ya kufikia ukubwa unaotakiwa maji yanaondolewa kwenye bwawa. Lakini miaka ya nyuma ufugaji samaki uneenea hadi baharini. Vizimbi vikubwa vinatengenezwa kwa seng'enge na kuzamishwa katika sehemu ya bahari pasipo hatari ya mawimbi makali kwa mfano katika hori nyembamba kama fyord za Norwei.


Samaki wanafugwa pia kama mapambo na kwa burudani na watu wanatua wale wenye rangi za pekee na kuwafuga hasa.

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: