Bonde la Ufa
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa Bonde la Ufa ni nafasi ya Ziwa Tanganyika
Kwenye fani ya jiolojia bonde la ufa ni bonde ambalo limeumbwa kutokana na mwendo wa mabamba ya gandunia mahali yanapoachana.
Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki ndiyo mojawapo ya mabonde maarufu zaidi duniani.
Mabonde ya ufa huumbwa kutokana na mvutano wa tektoniki. Mwendo huu huleta utengano wa mabamba hayo. Bonde la ufa latokea kama mabamba ya gandunia huachana na kuaha nafasi.
Mabonde ya ufa ni mahali ambako volkeno hujitokeza pamoja na matetemeko ya ardhi.
Mabonde ya ufa makubwa kabisa yapo chini ya maji kwenye misingi ya bahari.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bonde la Ufa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |