Algeria
|
|||||
| Wito la taifa: Kiarabu: من الشعب و للشعب
|
|||||
| Wimbo wa taifa: Kassaman (qasaman bin-nāzilāt il-māḥiqāt) (Arabic: Twayamini kwa radi inayoharibu) |
|||||
![]() |
|||||
| Mji mkuu | Algiers [1] |
||||
| Mji mkubwa nchini | Algiers | ||||
| Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
| Serikali | Demokrasia Jamhuri Abdelaziz Bouteflika Ahmed Ouyahia |
||||
| Uhuru Tarehe |
kutoka Ufaransa 5 Julai 1962 [2] |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
2,381,740 km² (11th) kidogo sana |
||||
| Idadi ya watu - 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
32,531,853 [1] (ya 36) 13/km² (ya 168) |
||||
| Fedha | Dinari ya Algeria (DZD) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CET (UTC(hawajali)) |
||||
| Intaneti TLD | .dz | ||||
| Kodi ya simu | +213
- |
||||
Algeria (pia: Aljeria ; kwa Kiarabu: الجزائر al-Jazā’ir) au kwa jina rasmi "Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Algeria" ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na bahari ya Mediteranea, Moroko, Sahara ya Magharibi, Mauretania, Mali, Niger, Libya na Tunisia.
Algeria ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika lakini sehemu kubwa ya eneo lake iko katika jangwa la Sahara.
Jina la nchi limetokana na mji mkuu unaoitwa kwa jina lilelile "al-jaza-ir" kama nchi ya leo kwa lugha ya Kiarabu.
Yaliyomo |
Historia [hariri]
Kwa lugha, utamaduni na historia Algeria ni sehemu ya dunia ya Kiarabu tangu miaka 1300 iliyopita. Nchi imebaki pia na idadi kubwa (25-30%) ya wakazi wa kabila la Waberber ambao kihistoria ni wenyeji asilia.
Mawe ya maghofu ya miji ya kale bado yanaonyesha uhusiano wake na Dola la Roma lililoitawala kwa karne nyingi hadi kuja kwa Waarabu.
Jiografia [hariri]
Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa, Sahara iko upande wa kusini. Asilimia 20 za eneo la Algeria katika kaskazini ni nyumbani kwa karibu wakazi wote. Maeneo haya ni pwani ya Mediteranea na milima ya Atlas.
Atlas inapanda hadi kimo cha mita 2,308.
Sahara inaanza kusini ya Atlas na kanda penye manyasi machache halafu inafuata eneo la matuta ya mchango pasipo na mimea yote. Tena kusini yake ni nyanda za juu ambazo ni hasa maeneo ya miamba matupu. Kwenye kusini kabisa kuna milima ya Ahaggar inayopanda hadi mita 2,918.
Mito ya kudumu iko kaskazini tu sehemu za pwani. Mabonde ya mito ya ndani ni pakavu isipokuwa baada ya mvua mito mikali inajitokeza kwa masaa kadhaa.
Hali ya hewa [hariri]
Kanda la kaskazini lina hali ya hewa inayoathiriwa na Bahari Mediteranea. Hapa halijoto kwenye mwezi wa Agosti ni 25 °C na 12 °C wakati wa Januari.
Kwenye sehemu za juu kuna baridi hata barafu kwenye majira ya Januari lakin i joto ni kali zaidi wakati wa Julai/Agosti.
Kusini ya Atlas inaanza hali ya hewa ya jangwani; halijoto inaweza kucheza zaidi ya 20 °C katika siku moja. Wakati wa joti halijoto inapita 40 °C lakini wakati wa baridi halijoto inashuka chini ya °C kwenye saa za usiku.
Mvua ni haba mno kuna miaka mfululizo bila tone moja. Katika milima ya Ahaggar kuna usimbishaji kidogo kutokana na ukungu kwa hiyo miti kadhaa na mimea mingine iko.
Historia [hariri]
Historia inayojuikana ilianza na Waberber ambao ni wenyeji asilia.
Tangu mwaka 1000 KK Wafinisia walianza kufika na kujenga miji yao ya biashara kwenye pwani ya Mediteranea. Muhimu kati ya miji yao ilikuwa hasa Karthago iliyopanua utawala wake hadi Hispania na Gallia (Ufaransa ya Kusini). Waberber wa bara walijenga milki zao za Numidia na Mauretania.
Katika vita kati ya Karthago na Roma ya Kale Waberber walisimama upande wa Roma wakapata uhuru wao kwa muda kidogo lakini wakati wa karne ya 1 KK Roma ilianza kutawala eneo la Algeria moja kwa moja.
Numidia na Mauretania zilikuwa mashamba ya Roma na sehemu kubwa ya nafaka za Italia zililimwa hapa. Utawala wa Roma ulivurugika baada ya Wavandali kutoka Ulaya Kaskazini kufika na kuanzisha milki yao kwa muda wa karne moja. Jeshi la Kaisari Justiniani I wa Bizanti ilirudisha utawala wa Kiroma, ila tu katika karne ya 7 uvamizi wa Waarabu Waislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma.
Kuanzia mwaka 642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutoka Misri walishambulia eneo la Afrika ya Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini baada ya uhamisho wa serikali ya makhalifa kutoka Medina kwenda Dameski] Waumawiya walikaza jitihada dhidi ya Afrika ya kaskazini.
Mwaka 670 jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji wa Kairuan kusini ya Tunis ya leo na mji huu ulikuwa kitovu cha unenezaji. Walipoenea katika Algeria ya leo walirudishwa na Waberber Wakristo kwa msaada wa Wabizanti lakini jeshi lililofuata lilishinda na kufikia mwaka 711 Afrika ya kaskazini yote (maana nchi za leo Tunisia, Algeria na Moroko) zilikuwa chini ya utawala wa Waarabu. Sehemu kubwa ya Waberber walifanya haraka kujiunga na Uislamu wakasaidiana na Waarabu.
Matokeo haya yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu maana yake upanuzi wa lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu.
Historia ya karibuni imeacha kumbukumbu yake inayoonekana katika athira kubwa ya lugha na utamaduni wa Kifaransa kutokana na ukoloni wa Ufaransa kati ya 1830 na 1962.
Kwa Marais wa nchi tangu uhuru, angalia hapa.
Kwa sasa Algeria inajenga upya umoja wa kitaifa baada ya vita kali ya wenyewe kwa wenyewe iliyoishia mwaka 2002.
Wilaya za Aljeria [hariri]
Kuna vitengo vya utawala 48 vinavyoitwa wilaya.
|
|
|
|
|
Miji [hariri]
Mascara-Oran
Algiers
Annaba
Temurssen
- ↑ 1.0 1.1 CIA World Factbook Algeria (accessed 4 Aprili 2006)
- ↑ Algeria County analysis Energy Information Administration (accessed 4 Aprili 2006)
Viungo vya Nje [hariri]
- Serikali
- El Mouradia official presidential site (in French and Arabic)
- National People's Assembly official parliamentary site
- Chief of State and Cabinet Members
- Maelezo zaidi
- Algeria entry at The World Factbook
- Algeria from UCB Libraries GovPubs
- Algeria katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Algeria
Algeria travel guide kutoka Wikisafiri- Photos From Algeria
- Ministère de l'Aménagement du Territoire, de l'Environnement et du Tourisme
- Map of Algeria
| Nchi za Afrika | |
|---|---|
| Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
| Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
| Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Algeria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
