Sentensi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

sentensi ni kipashio kikubwa cha kimuundo ambacho kimeundwa na kirai nomino(KN) na kirai kitenzi(KT) ambacho hutoa taarifa fulani. kimsingi kirai nomino kinamiundo mbalimbali katika lugha ya kiswahili. miundo hiyo ni kama vile;

  • Mfano wa nomino pekee:- mama anapika.
  • Mfano wa nomino na kivumishi:- kijana mrefu amepotea.
  • Mfano wa nomino na kibainishi:- juma bakari ni mwanafunzi.

Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.