Vivumishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
  • 'Kuku yule 'mweusi ametaga mayai kumi
  • Askari magereza amepigwa na mfungwa
  • 'Kaka unanipa hadithi ya kuvutia
  • Raia mwema amehama mtaa

Kivumishi ni neno/maneno yanayotoa taarifa ya ziada katika nomino. Kivumishi hufanya kazi ya kufafanua/kuelezea zaidi kuhusu nomino ili kupambanua/kuitofautisha nomino husika miongoni mwa nomino nyingine.

Kiwakilishi ni aina ya maneno ambayo husimama kuwakilisha nomino. Kivumishi hutoa taarifa ya ziada kuhusu nomino, kiwakilishi (endapo nomino haipo) au kivumishi chenzake (endapo kuna vivumishi zaidi ya kimoja katika tungo husika).

Mifano
  • Kijana yule ana tabia nzuri
  • Majumba kumi yamevunjika
  • Mawingu meusi yametanda angani
  • Yule mpole amesafiri
  • Bata mweupe ni wa jirani

Aina za vivumishi

  1. Vivumishi vya sifa
  2. Vivumishi vya idadi pia vya kiasi
  3. Vivumishi ya kuuliza
  4. Vivumishi vya kuonesha/Vivumishi vionyeshi/viashiria
  5. Vivumishi vya kumiliki
  6. Vivumishi vya -a unganifu
  7. Vivumishi vya urejeshi
  8. Vivumishi vya pekee
  9. Vivumishi vya jina kwa jina/nomino
  10. Vivumishi visisitizi

Inafanana kabisa na orodha ya viwakilishi, tofauti yake ni hali ya nafsi tu. Yaani, hakuna kivumishi cha nafsi.

Tazama pia

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vivumishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.