Nomino za dhahania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
  • Mzimu wa Kolelo
  • Usingizi umempitia
  • Hasira hasara
  • Shetani alaaniwe

Nomino za dhahania ni maneno yanayotaja majina ya watu na vitu ambavyo ni vya kufikirika tu. Ni dhana iliyomo ndani ya akili ya mzungumzaji. Watu na vitu hivyo huwezi kuvigusa wala kuviona kwa macho isipokuwa unaweza kuvifahamu kupitia milango ya fahamu tu.

Mifano
  • Upepo mkali umetokea kaskazini mwa bahari ya Hindi
  • Kumetokea na wizi katika nyumba ya jirani
  • Wivu ukizidi unakera
  • Mungu ndiye muumba wa vyote
  • Hewa chafu inatokea upande kushoto

Tazama pia

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nomino za dhahania kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.