Mofimu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mofimu katika sarufi ni jina la sehemu ndogo kabisa yenye kuwakilisha maana katika neno.
[hariri] Mifano
- "msemaji" lina mofimu nne ndani yake:
- "m" - ni mofimu ya nafsi
- "sem" - ni kiini cha tendo
- "a" - inaonyesha nia
- "ji" - inaonyesha mazoea
- "nimefika" lina pia mofimu nne ndani yake:
- "ni" - ni mofimu ya nafsi
- "me" - ni mofimu ya wakati
- "fik" - ni kiini cha tendo
- "a" - inaonyesha nia