Sarufi
Sarufi ni elimu ya kupanga maneno kwa ufasaha. Maneno hayo yanaweza kutafsiriwa kwa namna mbili tofauti. Mosi, yanaweza kutafsiriwa kwa maana ya ufunzaji wa vipengele kama msamiati, utungaji wa sentensi, viashiria, vitenzi na kadhalika. Hapa kuna mambo kama methali, hadithi, vitendawili, itikadi na kadhalika. Basi huachiwa mbali. Tafsiri ya pili ya maelezo haya huchukua yote yafunzwayo yote katika lugha fulani. Kama maelezo ya awali, sarufi ina vipengele tafauti tofauti. Ikiwa pamoja na kufunza maneno magumu, vitenzi, nyakati, matamshi, ngeli, vivumishi, majina, vielezi na viingizi. Tena, sarufi ni tawi la isimu.
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.