Homo
Homo ni jenasi inayojumlisha binadamu na spishi zinazofanana sana naye.
Jina homo ni la Kilatini, likiwa na maana ya "mtu", na kiasili linahusiana na neno "ardhi".[1]
Jenasi hiyo inakadiriwa kuanza kuwepo walau miaka 2.3 milioni iliyopita[2][3] kutokana na australopithecine.
Spishi ya kwanza ya jenasi hiyo ni ile ya Homo habilis, anayefikiriwa kutokana na Australopithecus garhi. Lakini mnamo Mei 2010 yalipatikana mabaki ya Homo gautengensis, spishi inayofikiriwa kuwa ya kale kuliko Homo habilis.[4]
Kutokana na Homo habilis walipatikana Homo ergaster, Homo erectus, Homo georgicus, Homo antecessor, Homo rhodesiensis, Homo heidelbergensis n.k.
Homo neanderthalensis na mtu wa Denisova labda ni nususpishi za Homo sapiens zilizoweza kuzaliana na watu waliotokea Afrika.[5][6][7]
Spishi zote za jenasi Homo zimekoma, isipokuwa Homo sapiens (binadamu).
Tanbihi [hariri]
- ↑ dhghem The American Heritage Dictionary of the English Language: Fourth Edition. 2000.
- ↑ Stringer, C.B. (1994). "Evolution of early humans", The Cambridge Encyclopedia of Human Evolution. Cambridge: Cambridge University Press, 242. ISBN 0-521-32370-3. Also ISBN 0-521-46786-1 (paperback)
- ↑ McHenry, H.M (2009). "Human Evolution", Evolution: The First Four Billion Years. Cambridge, Massachusetts: The Belknap Press of Harvard University Press, 265. ISBN 978-0-674-03175-3.
- ↑ "Toothy Tree-Swinger May Be Earliest Human"
- ↑ Green RE, Krause J, et al. A draft sequence of the Neandertal genome. Science. 2010 7 Mei;328(5979):710-22. doi:10.1126/science.1188021 PMID 20448178
- ↑ ^ Reich D, Green RE, Kircher M, et al. (Desemba 2010). "Genetic history of an archaic hominin group from Denisova Cave in Siberia". Nature 468 (7327): 1053–60. doi:10.1038/nature09710. PMID 21179161.
- ↑ Reich D ., et al. Denisova admixture and the first modern human dispersals into southeast Asia and Oceania. Am J Hum Genet. 2011 Oct 7;89(4):516-28, doi:10.1016/j.ajhg.2011.09.005 PMID 21944045.
- Serre et al. (2004). "No evidence of Neandertal mtDNA contribution to early modern humans". PLoS Biology 2 (3): 313–7. doi:10.1371/journal.pbio.0020057. PMC 368159. PMID 15024415.