Bonobo
| Sokwe Mtu Mdogo au Bonobo | ||||||||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Sokwe Mtu Mdogo au Bonobo
|
||||||||||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||||
|
Sokwe Mtu Mdogo au Bonobo ni jina la nyani wakubwa wa familia Hominidae wanaofanana sana na binadamu. Anatazamiwa kama spishi ya karibu zaidi na binadamu (Homo sapiens).
Spishi hii inaishi pekee katika eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa kaskazini ya mto Kongo katika eneo la Mkoa wa Equateur.
Bonobo imetazamiwa kwa muda mrefu kama aina ya pekee ya Sokwe Mtu wa Kawaida (Chimpanzee) akiitwa kwa majina kama chimpanzee mdogo. Lakini tangu utafiti wa mwanabilojia Mjerumani Ernst Schwarz mwaka 1928 na wenzake Waamerika Harold Coolidge na Robert Yerkes ilionekana ni spishi ya pekee ndani ya jenasi ya Pan.
Bonobo ni spishi katika hatari ya kupotea akiishi katika maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pekee. Wataalamu wameona ya kwamba spisho zote za Pan hawajui kuogelea vema kwa hiyo kuna hoja kuwa spishi zote mbili ziliachana baada ya kutokea kwa to Kongo takriban miaka milioni 1.5 – 2 iliyopita. Bonobo huishi kusini wa mto Kongo lakini Sokwe Mtu wa kawaida huishi pande wa askazini wa mtu huo.
Bonobo huwa na miguu mirefu, midomo yenye rangi ya pinki na uso mweusi. Nyele juu ya kichwa zinaelea upande kuanzia katikati juu ya kichwa. Kwa jumla katika jamii zao kike mzee ana nafasi kubwa.
Wanakula hasa matunda na majani lakini wanaongeza nyama kutoka wanyama wadogo.