Karolo Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sarafu ya mwaka 814 inayomwonyesha Karolo Mkuu
(Maandishi yanasema: "KAROLUS IMPAUG" yaani Karolus Imperator Augustus.
Karolo Mkuu na Papa Adrian I.

Karolo Mkuu (kwa Kilatini: Carolus Magnus; kwa Kijerumani: Karl der Große; kwa Kifaransa: Charlemagne) alizaliwa tarehe 2 Aprili mwaka 742 na kufariki tarehe 28 Januari 814; alikuwa kwanza mfalme wa Wafranki halafu Kaizari wa Dola takatifu la Roma aliloanzisha.

Pengine anaitwa "baba wa Ulaya" kwa kuwa milki yake iliunganisha nchi zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya (chanzo cha Umoja wa Ulaya) katika karne ya 20.

Tangu kale anaheshimiwa na baadhi ya Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Januari.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Wafranki walikuwa kabila la Kigermanik iliyofaulu kuvamia na kutawala sehemu kubwa za Gallia ya Kiroma.

Karolo alikuwa mwana wa mfalme wao Pippin mfupi akarithi nusu ya milki yake. Akaendelea kuunganisha nchi zote za Wafranki katika maeneo ya Ufaransa na Ujerumani ya leo baada ya kifo cha kaka yake kuanzia mwaka 786. Akaendelea tena kuvamia na kuteka nchi ya Wasaksoni kaskazini kwa Ujerumani.

Kwa njia ya ndoa (774) akajipatia pia taji la ufalme wa Lombardia katika Italia ya Kaskazini.

Akiwa na athira kubwa katika Italia pamoja na Ufaransa na Ujerumani akapewa cheo cha Kaizari na Papa Leo III wa Roma. Kwa njia hiyo alianzisha upya cheo cha Kaizari wa Roma katika magharibi.

Mwishoni milki yake iliunganisha maeneo ya Ufaransa, Ujerumani magharibi, Uholanzi, Ubelgiji, Luxemburg na Italia kaskazini ya leo.

Ingawa hakujua hata kusoma na kuandika alipenda elimu akaanzisha shule kadhaa.

Alipokufa mwaka 814 mtoto wake Ludoviko alirithi ufalme kutoka kwake.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Karolo Mkuu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.