Papa Leo III
Papa Leo III (takriban 750 – 12 Juni, 816) alikuwa papa kuanzia tarehe 26 Disemba, 795 hadi kifo chake. Alimfuata Papa Adrian I.
Leo III amejulikana kwa tendo lake la kumwekea Karolo Mkuu taji la Kaisari wa Roma tarehe 25 Desemba, mwaka wa 800.
Yeye mwenyewe alizaliwa katika familia raia aliona upinzani mkali baada ya uchaguzi wake kutoka familia za makabaila wa mji wa Roma waliojaribu kumwua kwa sababu makabaila walizoea kuwa na athira juu ya uchaguzi wa Papa wakati ule. Hivyo Leo alikimbia hadi Ujerumani akitafuta usaidizi wa Karolo mfalme wa Wafranki. Karolo alimrudisha Roma na walinzi, akafika mwenyewe kuchungulia mashtaki dhidi ya Leo III. Aliona mashtaki dhidi yake yalikuwa ya uwongo.
Leo III kwa upande wake alijaribu kuimarisha uhusiano wake na Karolo kwa kumwekea taji la Kaisari. Hivyo Karolo alikuwa mtu wa kwanza wa kutumia cheo hiki katika mji wa Roma tangu 476 mwaka Kaisari wa mwisho Romulus Augustus alipofukuzwa, na cheo cha Kaisari wa Roma kilipatikana huko Konstantinopoli tu kwa mtawala wa Bizanti. Tendo la kumwekea Karolo taji hilo lilimkasirisha kiongozi wa Konstantinopoli lakini alikosa nguvu ya kumwadhibu Papa au Karolo. Hivyo Leo III alianzisha ufuatano wa makaisari wa "Dola Takatifu la Roma" ulioendelea hadi mwaka wa 1804.
Leo III alitangazwa kuwa mtakatifu mwaka wa 1673.
[hariri] Viungo vya nje
Kuhusu Papa Leo III katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
| Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Leo III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |