Mkoa wa Rukwa
| Mkoa wa Rukwa |
|
| Nembo ya Tanzania | |
| Mahali pa Mkoa wa Rukwa katika Tanzania | |
| Anwani ya kijiografia: 7°0′S 31°30′E / 7°S 31.5°E | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Wilaya | 4 |
| Mji mkuu | Sumbawanga |
| Serikali | |
| - Mkuu wa Mkoa | Daniel Ole Njoolay |
| Eneo | |
| - Mkoa | 75,240 km² |
| Idadi ya wakazi (2002) | |
| - Mji | 1,141,743 |
| Tovuti: http://www.rukwa.go.tz/ | |
Rukwa ni moja kati ya mikoa 30 za Tanzania. Inapakana na mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi upande wa Kaskazini, mkoa wa Mbeya upande wa mashariki, Zambia kusini na upande wa magharibi Ziwa la Tanganyika lililo mpaka na Kongo pia. Makao makuu ya mkoa ni Sumbawanga.
Kabla ya kumegwa mwaka 2012 eneo la mkoa lilikuwa takriban 70,000 km². Kusini mwa mkoa liko ziwa la Rukwa ambalo ni kati maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki.
Wilaya [hariri]
Wilaya nne zilikuwa (idadi ya wakazi katika mabano): Sumbawanga Mjini (147,483), Sumbawanga Vijijini (373,080), Mpanda (412,683) na Nkansi (208,497).
Mwaka 2012 ilianzishwa wilaya ya Kalambo.
Wakazi [hariri]
Kulikuwa na wakazi 1,141,743 (sensa 2002), kwa asilimia kubwa waumini wa Kanisa Katoliki.
Kabila kuwba zaidi mkoani ndio Wafipa walioko hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkansi. Kati ya makabila mengine kuna Wamambwe-Lungu, Wawanda na Wanyamwanga katika wilaya ya Sumbawanga; kuna pia Wasukuma, Wanyamwezi na Wamassai.
Viungo vya nje [hariri]
Matokeo ya sensa 2002: en [1]
Makabila na lugha za Tanzania: en [2]
|
|
|
|---|---|
| Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Rukwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |