Mkoa wa Singida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Mkoa wa Singida katika Tanzania.

Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania: mkoa huo upo kanda ya kati, ukipakana na mikoa ya Manyara upande wa kaskazini, Dodoma mashariki, Iringa na Mbeya kusini, Tabora upande wa magharibi na Shinyanga.

msimbo wa posta ni 43000.

Kuna wilaya saba za Iramba, Manyoni, Singida Vijijini na Singida Mjini, Ikungi, Itigi na Mkalama.

Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa wakazi 2,008,058 [1]. kutoka 1,370,637 wa mwaka 2012[2].

Wakazi wa wilaya za Singida mjini na kijijini ni hasa Wanyaturu. Walio wengi Iramba ndio Wanyiramba na wakiwa Wagogo wengi huko Manyoni. Pia kati ya wenyeji kuna Wanyisanzu na makabila mengine madogo. Makabila hayo wanaishi kwa amani na upendo.

Lugha kuu ni Kiswahili, lakini pia kila kabila wanaongea yao.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Singida ni kati ya maeneo maskini zaidi ya Tanzania. Uchumi wake ni hasa ufugaji: idadi ya ng'ombe hukadiriwa kuwa takribani milioni 1.4. mbali na punda, kondoo, kuku. Masoko hayako karibu na barabara si nzuri.

Kilimo si kizuri kwa sababu ya hali ya mvua. Ukame huleta njaa. Singida ni kati ya mikoa inayotegemea misaada ya chakula. Kati ya mazao yapo ya chakula na ya biashara. Mazao yanayolimwa mkoani hapo ni mtama, alzeti, vitunguu, uweli, viazi, mahindi, karanga, maharage n.k.

Pamoja na kuwa mkoa wa Singida umekuwa ukikumbwa na njaa kwa sababu ya ukame, na hata pale mvua inaponyesha ni duni sana, una shughuli mbalimbali ambazo zinaingiza kipato kwa watu wa mkoa huo.

Ikiwa kuanzia miaka ya 1990 na kuendelea mpaka sasa imekuwa madini ya dhahabu yakigunduliwa katika sehemu mbalimbali mkoani Singida japo kumekuwa aidha hakufanyiwi uchunguzi wa kina kuhakiki kiwango cha hifadhi ya madini iliyopo katika eneo husika au huwa kiwako kilichopo ni kidogo, hivyo kutokuvutia wawekezaji wakubwa katika maeneo hayo. Kati ya madini ambayo yamewahi kugunduliwa katika mkoa wa Singida ni dhahabu ambayo imewahi kugunduliwa huko Londoni na Iruma wilayani Manyoni.

Mkoani Singida kuna mapori mengi ya akiba ambayo yamejaa wanyama wa aina nyingi ambao kama mapori hayo yatafanywa kuwa hifadhi kamili za taifa yangesaidia sana kuvutia utalii na kuufanya mkoa wa Singida uongeze pato lake na kupunguza umaskini miongoni mwa wanajamii kwani utatoa ajira kwa jamii inayozunguka hifadhi hizo.

Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Singida bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Singida kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.