Mkoa wa Morogoro
| Mkoa wa Morogoro |
|
| Nembo ya Tanzania | |
| Mahali pa Mkoa wa Morogoro katika Tanzania | |
| Anwani ya kijiografia: 8°0′S 37°0′E / 8°S 37°E | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Wilaya | 7 |
| Mji mkuu | Morogoro |
| Serikali | |
| - Mkuu wa Mkoa | Issa Machibya |
| Eneo | |
| - Mkoa | 73,039 km² |
| Idadi ya wakazi (2002) | |
| - Mji | 1,759,809 |
| Tovuti: http://www.morogoro.go.tz/ | |
Morogoro ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania.
Mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Umepakana na mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi, Ruvuma, Iringa, Dodoma na Arusha. Eneo lake ni 72 939 km², ambapo kuna wakazi 1,759,809 (mwaka 2002). Morogoro ni kati ya mikoa mikubwa zaidi ya Tanzania.
Yaliyomo |
[hariri] Utawala
Mkoa una wilaya sita ndizo (idadi ya wakazi kwa mabano): Kilosa ( 489,513), Kilombero (322,779), Morogoro Vijijini (263,920), Morogoro Mjini (228,863), Mvomero (260,525), Ulanga (194,209). Mwaka 2012 imeongezwa wilaya mpya ya Gairo.
Wakazi walio wengi hukalia wilaya za kaskazini. Robo yao huishi katika miji ya mkoa.
|
Wilaya za Mkoa wa Morogoro
|
||||||
|---|---|---|---|---|---|---|
| Ramani | Wilaya au manisipaa | Wakazi (2002) | Tarafa | Kata | Kijiji | Eneo km² |
| Wilaya ya Kilombero | 321,611 | 5 | 19 | 81 | 14,918 | |
| Wilaya ya Kilosa | 489,513 | 9 | 37 | 164 | 14,245 | |
| Wilaya ya Morogoro Vijijini | 263,920 | 6 | 25 | 132 | 11,925 | |
| Wilaya ya Morogoro Mjini | 227,921 | 1 | 19 | - | 531 | |
| Wilaya ya Mvomero | 260,525 | 4 | 17 | 101 | 7,325 | |
| Wilaya ya Ulanga | 193,280 | 5 | 24 | 65 | 24,560 | |
| Jumla | 1,759,809 | 30 | 141 | 543 | 73,039 | |
| Makisio ya idadi ya watu kwa mwaka 2008 ni watu 2,021,714 kutokana na kiwango cha ongezeko la watu la asilimia 2.6 kwa mwaka. |
||||||
| Marejeo: Mkoa wa Morogoro | ||||||
[hariri] Eneo
Eneo la Mkoa wa Morogoro liko katikati ya mikoa ya pwani ya Bahari Hindi na Nyanda za Juu.
Kuna tambarare za chini kama vile Ifakara / Kilombero, pia milima ya juu kama Uluguru penye mlima wa Kimhandu wenye 2646 m juu ya UB.
Mito mikubwa ni Wami na Ruvu inayoanza kwenye milima ya Uluguru. Ruvu ndiyo mto wa kutoa maji ya Daressalaam.
Karibu nusu ya eneo la Mkoa wa Morogoro ni hifadhi za wanyama za Mikumi na Udzungwa na sehemu ya eneo la kuwinda wanyama la Selous.
[hariri] Wakazi
Kabila kubwa ni la Waluguru waliotoa jina kwa mji wa Morogoro pamoja na milima ya Uluguru.
Makabila mengine makubwa zaidi ni Wangulu, Wakagulu, Wasagala, Wapogolo, Wandamba, Wabena, Wambungu na Wavidunda.
Upande wa dini, karibu nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo.
[hariri] Mawasiliano
Barabara Kuu za lami za Daressalaam - Morogoro - Mbeya - Zambia/Malawi na Daressalaam - Morogoro - Dodoma hupita eneo la mkoa pamoja na reli ya kati Daresalaam - Morogoro - Dodoma - Kigoma / Mwanza. Reli ya TAZARA hupita wilaya ya Kilombero.
[hariri] Uchumi
Kilimo kinategemea hali ya mvua. Kilombero kuna mashamba makubwa ya miwa. Mazao ya sokoni hulimwa milimani. Karibu nusu ya eneo la mashamba yote hulimwa mahindi.
[hariri] Marejeo ya Nje
|
|
|
|---|---|
| Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |