Mkoa wa Arusha
| Mkoa wa Arusha |
|
| Mlima Ol Doinyo Lengai karibu na kijiji cha Ngare Sero, Mkoa wa Arusha. | |
| Mahali pa Mkoa wa Arusha katika Tanzania | |
| Anwani ya kijiografia: 3°0′S 36°0′E / 3°S 36°E | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Wilaya | 6 |
| Mji mkuu | Arusha |
| Serikali | |
| - Mkuu wa Mkoa | Isidori Shirima |
| Eneo | |
| - Mkoa | 86,100 km² |
| - Maji | 2,460 km² |
| Idadi ya wakazi (2002) | |
| - Mji | 1,288,088 |
| Tovuti: http://www.arusha.go.tz/ | |
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Imepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani ni kufuatana na mwendo wa saa: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara. Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa pili kwa Utajiri nchini Tanzania.
Wilaya zake ni Monduli, Longido, Arumeru, Arusha, Ngorongoro na Karatu. Makao makuu yapo Arusha mjini.
Eneo lake ni km za mraba 86,100 zikiwemo km² 2,460 za maji. Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (2,878 m) bado ni volkeno hai, Arusha ni volkeno ya kulala tangu mw. 1910. Mvua hunyesha kati ya millimita 1,800 mm kwa mwaka mlimani Arusha hadi 508 mm kwa mwaka katika maeneo makavu.
Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Barabara ya lami Dar Es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, Tarangire na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimajaro iko karibu.
Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti. Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.
Kati ya wakazi wa mkoa kiasili ndio Waarusha, Wameru, Wairaqw na Wamassai.
|
Wilaya za Mkoa wa Arusha
|
||||||
|---|---|---|---|---|---|---|
| Ramani | Wilaya au manisipaa | Wakazi (2002) | Tarafa | Kata | Kijiji | Eneo km² |
| Wilaya ya Arumeru | 514,651 | 2,896 | ||||
| Arusha mjini | 281,608 | 93 | ||||
| Wilaya ya Karatu | 177,951 | 3,300 | ||||
| Wilaya ya Monduli | 110,442 | 6,419 | ||||
| Wilaya ya Ngorongoro | 129,362 | 14,036 | ||||
| Jumla | 1,288,088 | 34,526 | ||||
| 2002 Wilaya ya Longido: 7,782 km²; Idadi ya wakazi: 74,074 |
||||||
| Marejeo: Mkoa wa Arusha | ||||||
Viungo vya nje [hariri]
|
|
|
|---|---|
| Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Arusha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |