Arusha (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Arusha
Arusha is located in Tanzania
Arusha
Arusha
Mahali pa mji wa Arusha katika Tanzania
Coordinates: 3°22′S 36°41′E / Expression error: Unexpected < operator Expression error: Unexpected < operator / Expression error: Unexpected < operator; Expression error: Unexpected < operator
Nchi Tanzania
Mkoa Arusha
Wilaya Arusha
Idadi ya wakazi (2005)
 - Mji 341,155
Mji wa Arusha
Arusha na mlima wa Meru

Mji wa Arusha ni kati ya miji kumi mikubwa ya Tanzania na makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Kuna wakazi 341,155 (mw. 2005 – kutoka mn. 50,000 mw. 1970). Eneo lake ni 1400m juu ya uwiano wa bahari likiwa karibu na mlima wa Meru (4565m). Utalii na kilimo ni mgongo wa uti wa uchumi. Kwa sababu ya idadi kubwa ya watalii mji umepachikwa jina la “Dar-es-Safari”. Kuna pia viwanda muhimu vya kahawa, kusaga nafaka, kusafisha ukonge, kukuza maua za kuleta nje, pombe ya bia.

Arusha ina nafasi muhimu katika Historia ya Tanzania na Afrika. Mji umeanzishwa na Wajerumani mnamo mw. 1899. Ndipo hapo ya kwamba wakoloni Waingereza walitoa sahihi hati ya kuitolea Tanganyika uhuru mw. 1961. Mw. 1967 chama tawala cha TANU kiliunga mkono Tamko la Arusha lililoanzisha kipindi cha Ujamaa. Kuanzia mw. 1967 hadi mw. 1977 Arusha ndipo makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hadi kuanguka kwa umoja huu. Tangu mw. 1995 Mahakama ya Kimataifa ya Ruanda ina makao hapo. Arusha ni makao makuu ya KKKT, ambayo ni ofisi kuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

[hariri] Viungo vya nje

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Arusha - Mkoa wa Arusha - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Baraa | Daraja Mbili | Elerai | Engutoto | Kaloleni | Kati (Arusha) | Kimandolu | Lemara | Levolosi | Ngarenaro | Oloirien | Sekei | Sokoni I | Sombetini | Terrat | Themi | Unga L.T.D