Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kiingereza: East African Community
Wito: Watu Moja Hatima Moja
Kiingereza: "One People One Destiny"
Wimbo wa taifa: EAC Anthem
Makao makuu Arusha, Tanzania
Lugha rasmi Kiingereza
Aina Shirika la kimataifa
Uanachama Bendera ya Burundi Burundi
Bendera ya Kenya Kenya
Bendera ya Rwanda Rwanda
Bendera ya Tanzania Tanzania
Bendera ya Uganda Uganda
Viongozi
 -  Mwenyekiti Yoweri Museveni
 -  Mwenyekiti wa Baraza Shem Bageine
 -  Rais wa Mahakama Harold Nsekela
 -  Spika wa Bunge Margaret Zziwa
 -  Katibu Mkuu Richard Sezibera
Bunge Bunge la EAC (EALA)
Maanzilisho
 -  Mara ya kwanza 1967 
 -  Kufutwa 1977 
 -  Mara ya pili 7 July 2000 
Eneo
 -  Jumla 1,817,700 km2
701,818 sq mi 
 -  Maji (%) 5.6
Idadi ya watu
 -  2010 makisio 133,100,000
 -  Density 77.6/km2
201/sq mi
Pato la Taifa makisio 2010 
 -  Total US$ 79.2 billion
 -  Per capita US$ 685
Saa za eneo CAT / EAT (UTC+2 / +3)
Tovuti
eac.int

Jumuiya ya Afrika Mashariki ni shirika la kimataifa lenye washirika kutoka Afrika ya Mashariki ambao ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.[1] Wakati kwa ujumla, mataifa wanachama kwa kiasi kikubwa ni katika neema ya Shirikisho la Afrika Mashariki uchaguzi usio rasmi unaonyesha kwamba Watanzania wengi (asilimia themanini (80%) ya wakazi wake) wana mtazamo wa kinyume.[2] Tanzania ina ardhi zaidi kuliko mataifa mengine yakiunganishwa , na baadhi ya Watanzania wana hofu ya unyakuzi wa ardhi na wakazi wa sasa wa mataifa mengine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.[3] [4] [5] Uhaba wa ardhi ni suala nyeti katika eneo la Afrika ya Mashariki, hasa nchini Kenya, ambako mapigano ya wenyewe kwa wenyewe upande wa Mlima Elgon mwaka wa 2007 yaliwaacha zaidi ya watu 150 wamefariki na kulazimisha takriban watu wengine 60,000 kugura makazi yao.[6]

Hatua kubwa ya kwanza katika kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki ni muungano wa forodha katika mataifa husika uliotiwa saini mnamo Machi 2004 na ulioanza kutumika tarehe 1 Januari mwaka wa 2005. Chini ya masharti ya mkataba, Kenya, ambayo ndiyo nchi inayopata mauzo bora zaidi nje ya nchi katika kanda ya Afrika Mashariki, itaendelea kulipa ushuru kwa bidhaa zake zinazoingia nchi zingine wanachama hadi mwaka wa 2010, kwa kiwango kinachopungua na wakati. Mfumo sawa wa ushuru utatumika kwa bidhaa kutoka nchi ambazo sio wanachama.

Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianzishwa mnamo mwaka wa 1967, lakini iliporomoka mwaka wa 1977,na kusababisha sherehe na furaha tele nchini Kenya.[7] Ilifufuliwa tena rasmi tarehe 7 Julai 2000.[8] Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mojawapo ya nguzo muhimu za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika. Mwaka 2008, Jumuiya ya Afrika Mashariki, baada ya mazungumzo na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) ilikubali kupanua eneo la biashara huria na kuwahusisha wanachama wote watatu.

Wanachama[hariri | hariri chanzo]

Kanda ya Afrika Mashariki imezunguka eneo la kilomita milioni moja nukta nane (1.8) mraba na pamoja ina wakazi wapatao milioni mia moja (100) ( Makisio ya Julai 2005) na maliasili nyingi. Tanzania imekuwa na historia ya amani tangu kunyakua uhuru,ikilinganishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshuhudiwa katika mataifa ya Kenya, Rwanda, Burundi, na Uganda. Wakati huu Afrika Mashariki inajaribu kudumisha utulivu na mafanikio katikati ya migogoro inayoendelea katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Pembe ya Afrika, na kusini mwa Sudan. Lugha nne muhimu katika eneo la Afrika Mashariki ni Kiswahili, Kiingereza, Kirundi na Kinyarwanda, ingawa Kifaransa kiimeenea pia.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kutoka kushoto kwenda kulia, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Mwai Kibaki wa Kenya na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakati wa mkutano wa nane wa Jumuiya ya Africa Mashariki mjini Arusha, Novemba 2006

Kenya, Tanzania na Uganda zimekuwa na historia ya ushirikiano tangu karne ya 20, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Forodha baina ya Kenya na Uganda mwaka 1917,Tanganyika ilijiunga mnamo mwaka wa 1927, katika Ubalozi wa Afrika Mashariki (1948-1961) , 'East African Common Services Organisation' (1961-1967) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (1967-1977).[9]

Mwaka wa 1977, Jumuiya ya Afrika Mashariki iliporomoka baada ya miaka kumi kutokana na madai ya Kenya kuwa na viti zaidi kuliko Uganda na Tanzania katika kamati za maamuzi,[10] huku kukiwa na kutokuelewana kulikosababishwa na udikteta chini ya Idi Amin wa Uganda, Usoshalisti huko Tanzania, na soko Huria nchini Kenya,[11] na wanachama hawa watatu wakapoteza ushirikiano wa miaka zaidi ya sitini na manufaa ya ukubwa wa jumuiya hii kiuchumi. Kila mmoja wa wanachama hawa ilimbidi kuanza kutoa huduma na kujenga viwanda ambavyo hapo awali vilikuwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Baadaye, Rais Moi wa Kenya, Mwinyi wa Tanzania, na Museveni wa Uganda walitia saini Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki huko Arusha, Tanzania, tarehe 30 Novemba 1993, na kuanzisha Tume ya Ushirikiano ya nchi hizi tatu. Shughuli ya kuzileta pamoja nchi nchi hizi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, utafiti na teknolojia, ulinzi, usalama, masuala ya kisheria na kimahakama ilianza.

Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa hatimaye imefufuliwa tena mnamo tarehe 30 Novemba 1999, wakati Mkataba wa kuanzishwa upya ulitiwa saini. Ilianza ufufuzi kabisa tarehe 7 Julai 2000, miaka 23 baada ya kuporomoka kwa Jumuiya ya kwanza.

Mipango ya Baadaye[hariri | hariri chanzo]

Mkataba huu huenda ukazaa matunda hivi punde huku kukiwa na mipango ya mwaka wa 2004 kuanzisha sarafu moja itakayotumika kote Afrika Mashariki, kati ya 2011 na 2015. Kuna pia mipango ya soko la pamoja na muungano wa kisiasa, Shirikisho la Afrika Mashariki, rais mmoja(kwanza kwenye msingi wa mzunguko ) na baadaye bunge moja mwaka wa 2010. Hata hivyo, baadhi ya wataalamu kama KIPPRA, wanaonelea kuwa mipango hii haiwezi kufaulu kabla ya mwaka wa 2010 ukizingatia kwamba bado kuna changamoto za kijamii na kiuchumi ambazo bado hazijashughulikiwa.

Visa Moja kwa Watalii[hariri | hariri chanzo]

African Union
Map of the African Union with Suspended States.svg

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
the African UnionNchi zingine · Atlasi

Ilikuwa ni matarajio ya wengi kuwa kabla ya 2006 kungekuwa na Visa moja kwa watalii wote wanaozuru Afrika Mashariki, iwapo mpango huo ungeidhinishwa na mamlaka ya sekta husika chini ya Jumuiya hii. Iwapo ingekubalika basi Visa hii ingetumika kote katika ardhi ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda). Chini ya pendekezo hili Visa yoyote mpya ya Afrika Mashariki inaweza kupokelewa kutoka ubalozi wowote katika eneo la Afrika Mashariki.

Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Mahakama ya Afrika Mashariki ndiyo mahakama inayosimamia mambo ya kesi zote za kisheria katika eneo hili . Kwa muda sasa imo mjini Arusha, Tanzania.

Bunge la Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Bunge la Afrika Mashariki ndicho kitengo cha kutengeneza sheria katika eneo la Afrika Mashariki. Ina wajumbe 27 ambao wote wamechaguliwa na Bunge za nchi wanachama wa Jumuiya. Inahusika na masuala yote ambayo yanahusu Jumuiya hii kama vile kujadili bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kujadili masuala yote yanayohusu Jumuiya na kutoa mapendekezo kwa Baraza juu ya mambo wanayoyadhani muhimu kwa utekelezaji wa mkataba, kushirikiana pamoja na na Bunge husika na kuanzisha kamati kwa makusudi kama vile wanavyodhani ni muhimu. Tangu uzinduzi wake mnamo mwaka wa 2001,bodi hii aimekuwa na makao kadhaa mjini Arusha, Kampala na Nairobi.

Pasipoti ya Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka wa 2006. Rwanda ilijiunga na Jumuiya ya Afrika mashariki tarehe 1 Julai 2007

{Pasipoti ya Afrika Mashariki ilizinduliwa rasmi tarehe 1 Aprili 1999. {0/} Pasipoti ya Afrika Mashariki ilizinduliwa ili kurahisisha usafiri na kuvuka mipaka ya nchi husika.[12][13] Ni halali kwa kusafiri ndani ya eneo la Afrika Mashariki (Kenya,Uganda na Tanzania) na hivyo itakupa haki ya kuingia na kukaa kwa miezi sita katika nchi yoyote na kisha unaweza ukaitumia tena.[12] Pasipoti hii inatolewa katika nchi zote tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kenya, Uganda na Tanzania). Pasipoti hii inapatikana katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji katika miji ya Nairobi, Kampala na Dar es Salaam. Ni raia tu wa Afrika Mashariki wanaoweza kuomba kupewa pasipoti hii.[12][13] Gharama ya pasipoti hii ni dola 10 za Marekani au pesa sawa ukibadilisha kwa sarafu za nchi za Afrika mashariki.[13] Baada ya kujaza fomu za kupata pasipoti hii itachukua muda wa wiki mbili au tatu kuipata pasipoti yako tayari kwa matumizi. Ingawa pasipoti hii ni halali tu ndani ya Afrika Mashariki, majadiliano yalifanya hili kuwa na hati sawa za kusafiri kwa watu wote wa Afrika Mashariki kabla ya mwaka wa 2006.[12]

Mtandao Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya mtandao katika eneo la Afrika Mashariki bado uko chini mno ikilinganishwa na mataifa yaliyostawi kiuchumi. Eneo la Afrika Mashariki ni kituo kizuri cha kiuchumi huku ikikadiri kuwa ina wakazi zaidi ya milioni 120. Inakadiriwa kuwa asilimia 10 ya wakazi wa Afrika Mashariki -milioni 12 , huutumia Mtandao. Mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unasisitiza ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kwa kuzingatia uwezo wa kijamii. Wengi wa wakazi wa Afrika Mashariki hutumia mtandao kuangalia habari, kusoma barua pepe na kwenye mitandao ya kijamii mitandao mingine ya kijamii. Hivi karibuni kumekuwa na majukwaa mengi yanayoibuka katika eneo hili kwa lengo la kuileta pamoja Afrika Mashariki. Kasi ya mawasiliano kupitia kwa mtandao pia iko chini mno katika eneo la Afrika Mashariki, ikilinganishwa na mataifa yaliyostawi. Hii labda ni mojawapo ya vikwazo vya maendeleo ya mawasiliano ya mtandao Afrika Mashariki.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]