Madini
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
[[Faili:Pyrite.jpg|thumb|250px|Nyengwe (Pyrite) ni kampaundi ya chuma na sulfuri yenye fuwele nzuri]] Madini (Kiarabu معدن ma'adan) ni dutu mango inayopatikana duniani kiasili. Madini huwa na tabia maalumu wa kikemia, si mata ogania na huwa na muundo wa fuwele. Kwa lugha nyingine: Madini ni elementi au kampaundi ya kikemia inayoonyesha umbo la fuwele na ambayo imejitokeza kutokana na mchakato wa kijiolojia.
Kuna takriban madini 4,000 yaliyogunduliwa duniani. Miamba yote yanaundwa na madini na kuna hasa madini 30 yanayounda sehemu kubwa ya miamba duniani. Miamba kwa kawaida huwa na madini mbili au zaidi ndani yake.
Madini yapo kila mahali. Katika mazingira yetu kila jiwe limeundwa na madini. Ardhi ya shamba ina kiwango kikubwa cha madini ni punje za mchanga ambao ni mawe yaliyosagwa. Tukiwasha taa kuna madini kwenye uzi la kuwaka na umeme umefika kwenye taa kupitia shaba ya waya; na shaba hii ni madini. Seli za mwili wetu huhitaji madini na hivyo ni muhimu ya kwamba chakula chetu kina kiasi kidogo cha madini ya lazima kama chuma au kloridi.
Madini kadhaa hupendwa kama vito (johari, mawe ya thamani) au pia dhahabu.
[hariri] Viungo vya Nje