Mkoa wa Kagera
| Mkoa wa Kagera |
|
| Nembo ya Tanzania | |
| Mahali pa Mkoa wa Kagera katika Tanzania | |
| Anwani ya kijiografia: 1°55′S 31°18′E / 1.917°S 31.3°E | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Wilaya | 8 |
| Mji mkuu | Bukoba |
| Serikali | |
| - Mkuu wa Mkoa | Mohamed Babu |
| Eneo | |
| - Mkoa | 40,838 km² |
| - Bara | 28,953 km² |
| - Maji | 11,885 km² |
| Idadi ya wakazi (2002) | |
| - Mji | 2,003,888 |
| Tovuti: http://www.kagera.go.tz/ | |
Mkoa wa Kagera ni mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa katika Tanzania. Jina lake linatokana na mto Kagera.
Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mengine ya Tanzania ya Kigoma, Shinyanga na Mwanza. Eneo lake ni 28,953 km² za nchi kavu na 11,885 km² za maji hasa ya Viktoria Nyanza, jumla 40,838 km².
Mkoa wa Kagera uko mnamo 1000 m juu ya uwiano wa bahari.
Makao makuu ya mkoa ni mji wa Bukoba.
Kuna wilaya saba za Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Misenyi, Muleba, Karagwe, Ngara, Biharamulo na Kyerwa. Misenyi ni wilaya mpya iliyoanzishwa mwaka 2007 na Kyerwa ikafuata mwaka 2012.
Sensa ya mwaka 2002 imeonyesha idadi ya wakazi kuwa 2,003,888 inayoendelea kuongezeka asilimia 3.1% kwa mwaka.
External links [hariri]
- (Kiswahili) Tovuti wa Mkoa wa Kagera
- (Kiingereza) Kagera – Bukoba – the official webguide
- (Kiingereza) – Tourist Office Bukoba / Kagera
- (Kiingereza) United Republic of Tanzania: Kagera Region
- Utamaduni wa Kagera -en
|
|
|
|---|---|
| Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |