Wilaya ya Rorya
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rorya ni wilaya mpya katika mkoa wa Mara. Hadi 2006 ilikuwa sehemu ya magharibi ya wilaya ya Tarime. Makao Makuu ya Wilaya ya Rorya ni Ingri Juu.
Eneo la wilaya liko kati ya ziwa Viktoria Nyanza upande wa magharibi na Tarime upandwe wa mashariki. Upande wa kaskazini inapakana na Nchi ya Kenya na upande wa kusini wilaya ya Musoma.
Wakazi walio wengi ni Waluo.
Marejeo ya Nje[hariri]
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Rorya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
kigezo:Kata za Wilaya ya Rorya ni Bukura, Bukwe, Goribe, Ikoma, Kigunga, Kirogo, Kisumwa, Kitembe, Komuge, Koryo, Kyang'ombe, Mirare, Mkoma, Nyahongo, Nyamagaro, Nyamtinga, Nyamunga, Nyathorogo, Rabuor, Roche, na Tai