Mageuko ya spishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Mageuko ya spishi ni nadharia ya kisayansi iliyobuniwa na kutumiwa na wataalamu wa biolojia. Inasema ya kwamba spishi za viumbehai zilizopo duniani leo zimetokana na spishi zilizokuwa tofauti za zamani. Nadharia hii inategemea ya kwamba awali maisha yote yametokana na maumbo asilia. Katika wazo hili spishi zote jinsi zilivyo sasa zinaendelea kubadilika.

Msingi wa nadharia hii ni mabaki ya kisukuku ya viumbehai ambao hawapo tena duniani lakini wanaofanana kiasi na viumbehai wa leo, pamoja na ulinganifu wa spishi za karibu na mbali zaidi. Nadharia ya mageuko ya spishi inalenga kueleza mabadiliko haya.

Mtaalamu Mwingereza Charles Darwin anajulikana kama mfumbuzi wa nadharia hii.

Leo hii ni nadharia ya kibiolojia inayokubaliwa na wataalamu wengi hata kama kuna wapinzani kadhaa hasa upande wa wenye imani kali ya dini, lakini pia wachache kwa sababu za kitaalamu.

Mti wa uhai huonyesha mabadiliko wa spishi tangu mwanzo wa uhai

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: