Nikaragua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nikaragua


 • Eneo la jumlakm2
 • Eneo la ardhikm2
Ramani ya Nikaragua

Nikaragua (pia Nikaragwa) ni nchi ya Amerika ya Kati yenye wakazi 6,071,045 (2012). Imepakana na Honduras na Kosta Rika; upande wa magharibi ni pwani ya Pasifiki na upande wa mashariki kuna pwani ya Bahari ya Karibi.

Jina la nchi linasemekana kuwa mchanganyiko wa jina la wakazi asilia walioitwa "Nikarao" na neno la Kihispania la "agua" (=maji) kutokana na maziwa makubwa mawili nchini yanayoitwa Lago Managua na Lago Nicaragua. Maelezo mengine yanamtaja chifu wa wazalendo wakati wa kufika kwa Wahispania aliyeitwa "Nikarao".

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Nikaragua ina volkeno nyingi; nyororo ya milima ya kivolkeno hufuata mstari wa pwani ya Pasifiki.

Sehemu ya juu ni mlima Mogoton wenye kimo cha mita 2,438 juu ya UB.

Maziwa makubwa mawili ya maji matamu ni Lago Managua na Lago Nicaragua.

Eneo upande wa Karibi lina wakazi wachache sana: ni hasa eneo la misitu minene.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Nchi ilikuwa koloni la Hispania tangu mwaka 1524.

Mwaka 1821 iliachana na utawala wa Hispania pamoja na nchi jirani na kuingia katika Shirikisho la Amerika ya Kati.

Tangu mwaka 1854 imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi walio wengi sana hukalia maeneo ya mji mkuu Managua na pwani ya Pasifiki.

Sehemu kubwa (69 %) ni machotara kati ya wakazi asilia na Wazungu. 7% ni Wazungu. 9% wana asili ya Afrika, wakikaa hasa kwenye pwani Ya Bahari ya Karibi. Waindio ni asilimia 5.

Lugha rasmi na kubwa zaidi ni Kihispania, lakini si lugha pekee.

Upande wa dini, walio wengi ni Wakatoliki (61.5% kadiri ya sensa ya mwaka 2005) na Waprotestanti (30.6%). 15.1% hawana dini yoyote.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Taarifa za jumla
Sanaa na utamaduni
Mengineyo
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nikaragua kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Coordinates: 13°N 85°W / 13°N 85°W / 13; -85