Panama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
República de Panamá
Jamhuri ya Panama
Bendera ya Panama Nembo ya Panama
Bendera Nembo
Wito la taifa: Latin: Pro Mundi Beneficio
(Kilatini: Kwa salama ya dunia)
Wimbo wa taifa: Himno Istmeño
(Wimbo la shingo la nchi)
Lokeshen ya Panama
Mji mkuu Panama
8°58′ N 79°32′ W
Mji mkubwa nchini Panama
Lugha rasmi Kihispania (rasmi), Kiingereza na lugha za kieneyeji kwenye pwani la Karibi
Serikali demokrasia
Ricardo Martinelli
Uhuru
kutoka Hispania
Kolombia

28 Novemba 1821
3 Novemba 1903
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
75,517 km² (ya 118)
2.9
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - Mei 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
3,232,000 (ya 133)
2,839,177
43/km² (ya 156)
Fedha Balboa (PAB)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-5)
(UTC-5)
Intaneti TLD .pa
Kodi ya simu +507

-


Ramani ya Panama

Panama ni nchi ya kusini ya Amerika ya Kati. Shingo la nchi la Panama hutazamiwa kuwa mpaka kati ya bara za Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini.

Imepakana na Kosta Rika na Kolombia; pwani la Bahari ya Karibi lipo upande wa kaskazini na pwani la Pasifiki upande wa kusini.

Nchi iko kwenye sehemu nyembamba kabisa ya Amerika ya Kati. Mfereji wa Panama hukata shingo la nchi na kufanya jina la Panama kujulikana kote duniani.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Baada ya ukoloni wa Hispania Panama ilikuwa sehemu ya kaskazini ya Kolombia. Majaribio mbalimbali ya uasi dhidi ya Kolombia kwa shabaha ya kuwa nchi ya pekee katika karne ya 19 hayakufaulu.

Mabadiliko makubwa yalikuja na ujenzi wa mfereji wa Panama. Utangulizi wake ulikuwa reli kutoka Colon upande wa Karibi kwenda mji wa Panama upande wa Pasifiki iliyojengwa 1855. Reli hii ilirahisisha safari kati ya Atlantiki na Pasifiki kwa watu na bidhaa vilivyoelekea watu ule kwenda Kalifornia. Watu wengi walikwenda Kalifornia miaka ile kwa sababu ya dhahabu iliyopatikana kule tangu 1848 na hapakuwa na reli kati ya pwani zotze mbili za Marekani wakati ule.

Colon, Panama.

Wakati wa mwisho wa karne ya 19 Marekani ilianza kujenga mfereji kati ya bahari mbili wa kukata shingo la nchi. Serikali ya Marekani iliona umuhimu wa kutawala njia hii. Ikasaidia Wapanama waliotaka kujitenga na Kolombia kwa kutuma manowari Colon iliyozuia jitihada za Kolombia za kukandamiza ghasia hii. 3 Novemba 1903 Panama ilitangaza uhuru wake na kufanya mkataba na Marekani. Panama ilikodisha mlia wa nchi kwa pande zote mbili za mfereji kwa Marekani; Marekani iliahidi kutunza uhuru wa Panama.

Hali halisi ukanda wa mfereji ilikuwa eneo la Kimarekani hadi 31 Desemba 1999 iliporudishwa kwa serikali ya Panama.

Viungo vya ndani[hariri | hariri chanzo]

Centroamerica politico.png Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Panama kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.