Bonaire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha kutoka angani ya Bonaire kubwa na ndogo.

Bonaire (au Boneiru) ni kisiwa cha Karibi, karibu na Aruba na Curaçao, kaskazini kwa pwani ya Venezuela (Amerika ya Kusini).

Ni sehemu ya pekee ya Uholanzi.[1][2]

Eneo lake, pamoja na kisiwa kidogo cha jirani kisicho na watu (Klein Bonaire), ni kilometa mraba 294.

Wakazi wa kudumu ni 17,408. Wengi wao huongea hasa Kipapiamentu (74.7%), halafu Kihispania (11.8%) na Kiholanzi (8.8%) ambacho ndicho lugha rasmi.

Mji mkuu ni Kralendijk.

Nyumba ya kimapokeo yenye uzio wa miba, inayotunzwa katika makumbusho ya Rincon

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali

Utalii

Uasili

Habari

WebCams

Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bonaire kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.