Martinique
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Martinique | |||
| Mahali pa Martinique katika Karibi | |||
|
|||
| Nchi | |||
|---|---|---|---|
| Mji mkuu | Fort-de-France | ||
| Eneo | |||
| - Mkoa | 1,128 km² | ||
| Tovuti: http://www.cr-martinique.fr/ | |||
Martinique ni kisiwa cha Antili Ndogo katika Bahari ya Karibi. Ni eneo la ng'ambo la Ufaransa na mkoa (departement)wa Ufaransa. Eneo lake ni 1,128 km². Idadi ya wakazi ni takriban lakhi 4. Takriban nusu wao ni wa asili ya Kiafrika ikiwa wazee wao walipelekwa hapa kama watumwa kwa ajili ya kazi za mashamba ya miwa. Kikundi kikubwa cha pili ni watoto wa Wahindi waliopelekwa Martinique kwa kazi ya mashamba baada ya mwisho wa utumwa.
Mji mkuu ni Fort-de-France. Miji mingine ni pamoja na Sainte-Anne na St. Pierre (iliyoharibiwa na mlipuko wa volkeno ya Mont Pelee mwaka 1902).
Martinique ni maarufu kwa muziki yake ya zouk. Mwanamuziki mashuhuri wa muziki hii ni Kassav.
Tazama pia [hariri]
- Guadeloupe ni eneo nyingine ya Ufaransa katika Bahari ya Karibi.
Viungo vya Nje [hariri]
| Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Martinique kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
