Kinyarwanda
Kinyarwanda ni lugha ya Kibantu ambayo ni lugha rasmi nchini Rwanda. Kuna wasemaji pia katika Uganda kusini na sehemu za mashariki za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Jumla ya wasemaji hukadiriwa kuwa mnamo milioni 7.
Wasemaji wa Kinyarwanda na Kirundi wanasikizana bila matatizo.
Mifano [hariri]
amakuru = Hujambo - hamjambo
amakuru ni meza = Sijambo / hatujambo
Muraho = Habari gani?
Wiriwe = Habari za mchana
ndagukunda = Nakupenda
murakoze = asante
vuba = haraka
kuririmba = kuimba
kurya = kula
icyayi = chai
Umugabo = mwanaume
Umugore = mwanamke
Umwana = mtoto / mwana
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kinyarwanda kwenye Multitree
- ramani ya Kinyarwanda
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=kin
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.