Kizulu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kizulu (isiZulu) ni lugha ya Wazulu inayoongelewa nchini Afrika Kusini na idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni 9-10 hasa katika jimbo la KwaZulu-Natal. Kizulu huhesabiwa kati ya lugha za Kinguni ndani ya lugha za Kibantu.
Wakati wa mfecane katika karne ya 19 wasemaji wa lugha ya Kizulu zimehama hadi Zimbabwe, Zambia, Msumbiji na Tanzania ambako lugha imebadilika kiasi kuwa kwa mfano Kindebele au Kingoni.
| Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kizulu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |