Jamhuri ya Dominika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
República Dominicana
Jamhuri ya Dominika
Bendera ya Jamhuri ya Dominika Nembo ya Jamhuri ya Dominika
Bendera Nembo
Wito la taifa: Kihispania: Dios, Patria, Libertad
( Mungu, Taifa, Uhuru)
Wimbo wa taifa: Quisqueyanos valientes
Lokeshen ya Jamhuri ya Dominika
Mji mkuu Santo Domingo
18°30′ N 69°59′ W
Mji mkubwa nchini Santo Domingo
Lugha rasmi Kihispania
Serikali Jamhuri
Leonel Fernández
Uhuru
TArehe
27 Februari 1844
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
48,442 km² (ya 131)
1.6
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 2002 sensa
 - Msongamano wa watu
 
8,895,000 (ya 87)
8,562,541
182/km² (ya 58)
Fedha Peso ya Dominika (DOP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-4)
(UTC)
Intaneti TLD .do
Kodi ya simu +1-809 and +1-829

-


Ramani ya Jamhuri ya Dominika

Jamhuri ya Dominika ni nchi kwenye kisiwa cha Karibi cha Hispaniola inayopakana na Haiti.

Hispaniola ni kisiwa kikubwa cha pili cha Antili Kubwa na iko upande wa magharibi ya Puerto Rico karibu na Kuba na Jamaica. Wenyeji hutumia jina la Quisqueya kwa ajili ya kisiwa chao ambacho ni neno la asili ya kitaino wenyeji asilia.

Mji mkuu pia mji mkubwa ni Santo Domingo.

Kihispania ni lugha rasmi na ya kawaida katika matumizi ya wananchi. Wengi wao ni wafuasi wa Yesu Kristo katika Kanisa Katoliki, ambalo lilianzisha humo jimbo lake la kwanza katika Amerika.

Uchumi unategemea kilimo na utalii.

Jina la nchi wakati mwingine linachanganywa na Dominica ambayo ni nchi nyingine katika kisiwa cha Karibi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Uso wa nchi ni wa milima mingi. Safu ya milima ya kati "Cordillera Central" ina milima ya juu kabisa ya Karibi kote ni Pico Duarte (3,175 m) na Loma Rucilla (3,039 m).

Hali ya hewa ni ya kitropiki lakini mlimani kuna baridi kali zaidi hadi ufikia chini ya 0°C.

Milima mingine ni:

  • safu ya "Cordillera Septentrional" katika kaskazini (hadi 1,249 m juu ya UB)
  • safu za "Cordillera Oriental" na "Costera del Caribe" katika mashariki (hadi 736 m juu ya UB)
  • milima ya "Sierra de Baoruco" katika kusini-mashariki (hadi 2,085 m juu ya UB)

Mito iko mingi lakini si mikubwa kama vile Higuamo, Romana, Yaque del Norte, Yaque del Sur, Yuna, Yuma, na Bajabonico. Kati ya visiwa vingi vidogo kuna viwili vikubwa kiasi ni Saona na Beata uupande wa kusini.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mianzo na koloni ya Hispania[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuja kwa Wahispania Hispaniola ilikaliwa na Waindio Waarawak wa kabila Wataino. Kristoforo Kolumbus alikanyaga ardhi ya Amerika mara ya kwanza katika eneo la Jamhuri ya Dominika. Nchi ilikuwa koloni ya Hispania kwa jina "Santo Domingo" ikabaki hivyo hata baada ya Ufaransa kununua theluthi ya magharibi ya kisiwa iliyokuwa Haiti baadaye.

Tangu 1510 Wahispania walianza kuleta watumwa Waafrika kama wafanyakazi kwenye mashamba makubwa hasa ya miwa. Wengi walitoroka wakakimbia na kuanzisha jumuiya huru za Wamaroni porini katika milima ya kisiwa. Hata kama leo zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wote wana uzazi wa kiafrika watumwa hawakuwepo wengi katika Santo Domingo jinsi ilivyokuwa upande wa Haiti chini ya utawala wa Ufaransa.

Utawala wa Haiti[hariri | hariri chanzo]

Santo Domingo ilitangaza uhuru wake tar. 30 Novemba 1821 baada ya kuona Hispania ilishindwa kote Amerika Kusini isipokuwa katika isipokuwa kwenye visiwa vya Karibi. Lakini baada ya wiki chache nchi ilivamiwa na jeshi al Haiti ikatawaliwa na Wahaiti kwa miaka 22. Utawala huo ulionekana kwa wenyeji kama utawala wa mabavu na kuanzia 1838 shirika ya siri ilifanya mipango ya kuwa nchi ya pekee tena.

Uhuru[hariri | hariri chanzo]

27 Februari 1844 wakati wa mapinduzi katika Haiti matajiri wa Santo Domingo walitangaza uhuru wa Jamhuri ya Dominika. Katika miaka iliyofuata Haiti ilijaribu kuvamia nchi mara tano na kurudisha utawala wake lakini watetezi walishinda.

Kurudi kwa Wahiapania[hariri | hariri chanzo]

Kati ya 1861 na 1865 rais Santana alikabidhi Dominika tena kwa Hispania kwa sababu aliamini ya kwamba nchi ilikosa nguvu ya kusimama pekee yake. Lakini raia wengine walipinga lurudi kwa Wahispania na kwa msaada wa kijeshi wa Haiti Wahispania walilazimishwa kuondoka.

Jamhuri ya pili[hariri | hariri chanzo]

Jamhuri ya Dominika iliendelea kuwa nchi dhaifu. Kati ya 1865 na 1879 serikali 21 zilihesabiwa pamoja matukio ya uasi wa kijeshi 50.

Mwisho wa karne ya 19 rais Ulises 'Lilís' Heureaux alikopa pesa nyingi kutoka benki za Ulaya lakini kutokana na kushiuka kwa bei ya sukari alishindwa kuilipia. Lakini nchi za nje zilidai pesa zilizokopwa.

Utawala wa Marekani[hariri | hariri chanzo]

Tangu Januari 1905 utawala wa ushuru uluchukuliwa na Marekani. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Marekani ilivamia kisiwa chote cha Hispaniola, kwanza Haiti, halafu pia Jamhuri ya Dominika. Utawala wa Marekani uliendelea hadi 1830.

Udikteta wa Trujillo[hariri | hariri chanzo]

Ilifuatwa na kipindi cha udikteta wa mkuu wa jeshi Rafael Leónidas Trujillo aliyechukua utawala kwa miaka 30 hadi ya kifo chake 30 Mei 1961. Alitawala kwa unyama na kupora mali ya umma.

Kipindi cha mapinduzi[hariri | hariri chanzo]

Rais Juan Bosch aliyefuata siasa ya ujamaa alichaguliwa 27 Februari 1963. Matajiri na serikali ya MArekani walihofia ya kwamba angefuata mfano wa Fidel Castro nchini Kuba akapinduliwa kwa msaada wa idara ya ujasusi wa Marekani CIA. Kipindi cha vita ya wenyewe kwa wenyewe kilifuata hadi Umoja wa Mataifa uliingilia kati na kutuma wanajeshi wa kurudisha amani.

Hadi wakati wa kisasa[hariri | hariri chanzo]

Katika Juni 1966 Joaquín Balaguer aliyewahi kuwa makamu wa rais Trujillo alichaguliwa kuwa rais. Uchaguzi huu ulikuwa na wasiwasi nyingi kama kura za baadaye. Katika miaka iliyofuata Balaguer alirudishwa hadi 1978. Baada ya vipindi vya marais wengine Balaguer alirudishwa tena 1986, 1990 na 1994.

Kura za mwisho baada ya Balaguer ziliteua maraisi Leonel Fernández Reyna, Hipólito Mejía na tena Leonel Fernández Reyna tangu 2004.


Caribe-geográfico.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Dominika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.