Damu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya darubini ya elektroni ya ukaguzi (SEM) ya seli nyekundu ya kawaida ya damu, chembe za kugandisha damu, na seli nyeupe za damu.
Mzunguko wa damu: Nyekundu = yenye oksijeni Buluu = bila oksijeni
Damu ya binadamu iliyokuzwa mara 600
Damu ya chura iliyokuzwa mara 600
Damu ya samaki iliyokuzwa mara 600
Damu ikitoka kwenye kidonda

Damu (kutoka neno la Kiarabu) ni kiowevu katika mwili wa binadamu na wanyama. Inazunguka mwilini ndani ya mishipa ya damu ikisukumwa na moyo kwa lengo la kumwezesha kuishi.

Kazi ya tishu hiyo ni kupeleka lishe na oksijeni kwa seli za mwili na kutoa daioksaidi ya kaboni pamoja na uchafu mwingine kutoka seli.

Ndani ya damu kuna utegili (kwa Kiingereza plasma) ambao ni kiowevu chake pamoja na seli za damu nyekundu na nyeupe. Seli nyekundu hubeba oksijeni wakati daioksaidi ya kaboni hubebwa na utegili. Seli nyeupe ni kama walinzi wa mwili wa kupambana na magonjwa. Pia kuna chembe sahani.

Mtu mzima huwa na damu lita 6 mwilini.

Muundo wa damu[hariri | hariri chanzo]

Kati ya viumbe wenye uti wa mgongo, damu imetengenezwa kwa seli za damu zinazoelea katika umajimaji unaoitwa plasma ya damu. Plasma, inayoundwa kwa 55% ya giligili ya damu, ambayo hasa ni maji (90% kwa kiasi), [1] na ina protini, glukosi, ioni za madini, homoni, dioksidi ya kaboni (Plasma ikiwa ndiyo chombo kikuu cha usafirishaji wa bidhaa taka), chembe za kugandisha damu na seli za damu zenyewe. Seli za damu zilizo kwenye damu hasa ni seli nyekundu za damu (zinazofahamika pia kama RBC yaani Red Blood Cells au erithrosaiti) na seli nyeupe za damu, zikiwa pamoja na lukosaiti na chembe za kugandisha damu.

Seli nyingi zaidi katika damu za wanyama wenye uti wa mgongo ni seli nyekundu za damu. Seli hizi zina himoglobini, protini yenye madini ya chuma, ambayo huwezesha usafirishaji wa oksijeni kwa kujiunganisha kwa hali ya kujirudia na gesi hii ya kupumua na kuongeza kwa kiasi kikubwa umumunyifu wake katika damu. Kwa upande mwingine, dioksidi ya kaboni inasafirishwa karibu kabisa nje ya seli ikiwa imeyeyushwa ndani ya plazma kama ioni ya bikaboneti.

Damu ya wanyama wenye uti wa mgongo huwa nyekundu yenye kung'aa wakati ambapo himoglobini yake imewekewa oksijeni. Wanyama wengine, kama vile krusteshia na moluska, hutumia hemosianini kubeba oksijeni, badala ya himoglobini. Wadudu na baadhi ya moluska hutumia ugiligili unaoitwa hemolimfu badala ya damu, tofauti ikiwa kwamba hemolimfu haipatikani katika mfumo wa usambazaji uliofungwa. Katika wadudu wengi, "damu" hii haina molekuli zinazobeba oksijeni kama vile himoglobini kwa sababu miili yao ni midogo na hivyo mfumo wao wa kupumua unatosha kusambaza oksijeni.

Wanyama wenye uti wa mgongo na walio pia na taya wana Mfumo wa kingamaradhi unaotegemea kwa kiasi kikubwa seli nyeupe za damu. Seli hizo husaidia kupinga maambukizi na vimelea. Chembe za kugandisha damu ni muhimu katika ugandishaji wa damu. [2] Athropodi, zinazotumia himolimfu, zina hemosaiti kama sehemu ya mfumo wao wa kinga.

Damu inasambazwa mwilini kupitia mishipa ya damu kutokana na usukumaji wa moyo. Katika wanyama wenye mapafu, damu kutoka kwa ateri hubeba oksijeni kutoka kwa hewa iliyovutwa hadi kwenye tishu za mwili, na damu kutoka kwa vena hubeba dioksidi ya kaboni, bidhaa taka zinazotokana na umetaboli, zinazozalishwa na seli, kutoka kwa tishu hadi kwa mapafu ili zitolewe.

Istilahi za uuguzi zinazohusiana na damu mara nyingi huanza kwa hemo- au hemato- (pia inaandikwa haemo- na haemato-) kutoka neno la Kigiriki cha Kale αἷμα, haima yenye maana ya "damu".

Kwa upande wa anatomia na histolojia, damu inafikiriwa kama muundo maalum wa tishu unganifu, kutokana na asili yake ya mifupa na uwepo wa nyuzi zenye mfumo wa fibrinojeni.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Himoglobinikijani = kikundi cha heme nyekundu & buluu = visehemu vya protini
Heme

Damu hufanya kazi nyingi muhimu katika mwili, zikiwemo:

  • Upelekaji wa oksijeni kwenye tishu (zilizoungana na himoglobini, ambayo hubebwa kwenye seli nyekundu)
  • Ugavi wa virutubishi kama vile glukosi, amino asidi, na asidi zenye mafuta (zilizoyeyushwa kwenye damu au zimeungana na protini za plazma (kwa mfano, lipidi za damu)
  • Uondoaji wa taka kama vile dioksidi ya kaboni, urea, na asidi ya maziwa yaliyochachuka
  • Kazi za kukinga mwili, ikiwa ni pamoja na mzunguko wa seli nyeupe za damu, na utambuzi wa vifaa vya nje kupitia zindiko
  • Kuganda, ambayo ni sehemu moja ya utaratibu wa kujirekebisha kwa mwili (ambapo damu huganda wakati mtu anapokatwa ili kuziba kutoka kwa damu)
  • Kazi za mjumbe, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa homoni na kutoa ishara ya uharibifu wa tishu
  • Udhibiti wa pH(kiwango cha uasidi au ualikali) mwilini
  • Udhibiti wa kiwango cha joto mwilini
  • Kazi za mwendo wa maji

Vipengele vya damu ya binadamu[hariri | hariri chanzo]

Neli mbili za EDTA-damu isiyoganda. Neli ya kushoto: baada ya kusimama, RBC zinakusanyika katika sehemu ya chini ya neli. Neli ya kulia: yenye damu mbichi iliyotoka kutolewa.

Damu inachangia 8% ya uzito wa mwili wa binadamu,[3] ulio na uzito wastani wa 1060 kg/ m 3, inakaribiana sana na uzito wa maji safi ya 1000 kg/m3. [4] Mtu mzima wa kadiri ana kiasi cha damu cha kama lita 5 (1.3 gal), linalojumuisha plazma na aina kadhaa za seli (zinazoitwa mara kwa mara chembedamu); elementi hizi zilizoundwa kutoka kwa damu ni chembechembe nyekundu (seli nyekundu za damu), lukosaiti (seli nyeupe za damu), na thrombositi (chembe za kugandisha damu). Kwa kiasi, seli nyekundu za damu huchangia takribani 45% ya damu yote, plazma takribani 54.3%, na seli nyeupe takribani 0.7%.

Damu yote (plazma na seli) huonyesha sifa zisizofuata sheria za giligili za Newton; sifa zake za kutiririka hubadilika ili kutiririka ipasavyo kupitia mishipa midogo ya damu kwa upinzani mdogo zaidi kuliko plazma ikiwa peke yake. Aidha, kama himoglobini yote ya binadamu ingekuwa huru katika plazma badala ya kuwekwa kwenye RBCs, giligili za mzunguko ungenata sana na kufikia kiwango ambapo unazuia utendakazi bora wa mfumo wa moyo na mishipa.

Seli[hariri | hariri chanzo]

Mikrolita moja ya damu ina:

  • Chembechembe nyekundu za damu milioni 4.7 hadi 6.1 (za kiume), milioni 4.2 hadi 5.4 (za kike): [5] Katika mamalia wengi, seli nyekundu za damu zilizokomaa zinakosa kiini na oganeli. Zina himogloboni za damu na husambaza oksijeni. Seli nyekundu za damu (pamoja na seli za vyombo vya endotheli na seli nyingine) pia zimetiwa alama na glaikoprotini ambazo zinatambulisha aina za damu tofauti. Kiwango cha damu kinachomilikiwa na seli nyekundu za damu kinajulikana kama hematokriti, na kwa kawaida ni takriban 45% ya damu. Ukubwa wa eneo la seli zote nyekundu za damu katika mwili wa binadamu zikiwekwa pamoja utakuwa takribani mara 2,000 kubwa zaidi ya sehemu ya nje ya mwili.[6]
  • Lukosaiti 4,000 hadi 11,000: [7] Seli nyeupe za damu ni sehemu ya mfumo wa kinga; zinaangamiza na kuondoa seli nzee au potovu na mabaki ya chembechembe, na pia hushambulia vikolezo vinavyoleta maambukizi (visababisha magonjwa) na dutu za kigeni. Kansa ya lukosaiti inaitwa lukemia.
  • Thrombosaiti 200,000 hadi 500,000: [7] thrombosaiti, ambazo pia hujulikana kama chembe za kugandisha damu, zina jukumu kugandisha damu (ugandishaji). Hubadilisha fibrinojeni iwe fibrini. Fibrini hii inaunda wavu ambayo seli nyekundu za damu hukusanyika juu yake na kuganda na hii kuzuia damu zaidi kutoka kwenye mwili na pia husaidia kuzuia bakteria kuingia mwili.
Maumbile ya damu ya kawaida
Kigezo Thamani
Hematokriti 45 ± 7 (38-52%) kwa wanaume
42 ± 5 (37-47%) kwa wanawake
pH 7.35-7.45
wigo besi -3 Na 3
P O 2 10-13 kPa (8-10 mm Hg)
P CO 2 4.8-5.8 kPa (35-45 mm Hg)
HCO 3 - 21-27 mm
Ulowesh(w)aji wa Oksijeni Iliyowekwa oksijeni: 98-99%
Iliyoondolewa Oksijeni: 75%

Plazma[hariri | hariri chanzo]

Takribani 55% ya damu yote ni plazma ya damu, giligili ambalo ni chombo cha majimaji cha damu ambalo lina rangi ya manjano ya nyasi. Kiasi cha jumla cha plazma ya damu katika mwili wa binadamu wastani ni lita 2.7 hadi 3.0. Kimsingi, ni mchanganyiko wa maji (92%) na protini (8%) na viwango vidogo vya vitu vingine.

Plazma hueneza virutubishi vilivyoyeyushwa, kama vile glukosi, asidi za amino, na asidi zenye mafuta (zilizoyeyushwa kwenye damu au zilizoshikana na protini za plazma), na huondoa bidhaa za taka, kama vile oksidi ya kaboni, urea, na asidi ya maziwa yaliyochachuka.

Sehemu nyingine muhimu ni pamoja na:

  • Albumini ya majimaji ya damu
  • Vipengele vya kugandisha damu (ili kuwezesha ugandishaji)
  • Globulini zinazokinga maradhi (kingamwili)
  • Chembe za lipoprotini
  • Protini nyingine
  • Elektrolaiti mbalimbali (hasa sodiamu na kloridi)

Neno seramu (majimaji ya damu) inarejelea plazma ambayo imetolewa protini za kuganda. Nyingi kati ya protini zilizobaki ni albumini na globulini zinazokinga maradhi.

Kadiri ndogo ya thamani za pH[hariri | hariri chanzo]

pH ya damu inadhibitiwa ili ibaki katika kadiri ndogo ya 7.35 hadi 7.45, na hivyo kuifanya alikalini kiasi. [8] [9] Damu iliyo na pH chini ya 7.35 ni ya asidi mno, huku pH ya damu iliyo juu ya 7.45 ni ya alkali mno. pH ya damu, sehemu ya shinikizo la oksijeni (po 2), sehemu ya shinikizo la dioksidi ya kaboni (pCO 2), na 3 HCO zinadhibitiwa kwa makini kupitia taratibu kadhaa za homiostasisi, ambazo hutumia uwezo wao hasa kupitia mfumo wa upumuaji na mfumo wa mkojo ili kudhibiti usawa wa msingi wa asidi na kupumua. Gesi ya damu ya ateri itapima vitu hivi. Plazma pia huzungusha homoni na kupeleka ujumbe wao kwa tishu mbalimbali. Orodha ya kadiri za kurejelea za kawaida za elektrolaiti mbalimbali ni ndefu.

Mifupa hasa huathiriwa na pH ya damu kwa kuwa mara kwa mara hutumika kama chanzo cha madini kwa kukinga pH. Kula kiasi kikubwa cha protini za wanyama na protini ya mimea huhusishwa na kupotea kwa mifupa kwa wanawake. [10]

Damu katika wanyama wenye uti wa mgongo wasio binadamu[hariri | hariri chanzo]

Damu ya binadamu inafanana na ile ya mamalia, ingawa maelezo sahihi kuhusu idadi ya seli, ukubwa, muundo wa protini na kadhalika, huwa tofauti kiasi kati ya aina tofauti ya mamalia. Hata hivyo, kati ya wanyama wenye uti wa mgongo wasio katika kategoria ya mamalia, kuna tofauti kadhaa muhimu: [11]

  • Seli za damu za wanyama wenye uti wa mgongo wasio mamalia zimetandazwa na zina umbo la yai, na huhifadhi viini vya seli zao
  • Kuna tofauti kubwa katika aina na idadi ya seli nyeupe za damu; kwa mfano, asidofili kwa jumla hupatikana zaidi kuliko kwa binadamu
  • Chembe za kugandisha damu zinapatikana tu kwa mamalia; katika wanyama wengine wenye uti wa mgongo, seli ndogo, zenye kiini, za spindu zinashughulikia kuganda kwa damu badala yake

Fiziolojia[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa moyo na mishipa[hariri | hariri chanzo]

Mzunguko wa damu kupitia moyo wa binadamu

Damu husambazwa mwilini kupitia vyombo vya damu kwa msukumo wa moyo. Kwa binadamu, damu husukumwa kutoka ventrikuli thabiti ya kushoto ya moyo na kupitia ateri hadi tishu za pembeni na hurudi kwa atiria ya moyo kupitia mshipa. Baadaye huingia kwenye ventrikali ya kulia kupitia ateri ya mapafu na husukumwa kwa mapafu na kurudi kwenye atiria ya kushoto kupitia mshipa wa mapafu. Damu kisha inaingia katika ventrikali ya kushoto ili isambazwe tena. Damu ya ateri hubeba oksijeni kutoka kwa hewa iliyovutwa ndani hadi kwa seli zote za mwili, na damu ya vena hubeba dioksidi ya kaboni, bidhaa taka ya metaboli ya seli, hadi kwa mapafu ili itolewe nje. Hata hivyo, tofauti moja ni ile ya ateri ya mapafu, iliyo na damu isiyo na oksijeni zaidi mwenye mwili, huku vena za zikiwa na damu yenye oksijeni.

Mtiririko wa ziada wa kurudi unaweza kutokana na kusongezwa kwa misuli ya kiunzi cha mifupa ambazo zinaweza kubana vena na kusukuma damu kupitia vali katika vena kuelekea ateri ya kulia.

Mzunguko wa damu ulielezwa kwa umaarufu na William Harvey katika mwaka wa 1628. [12]

Uzalishaji na uchakaaji wa seli za damu[hariri | hariri chanzo]

Katika wanyama wenye uti wa mgongo, seli mbalimbali za damu huundwa katika uboho kupitia mchakato unaoitwa hematopoiesia, unaohusisha erithropoesisi, uzalishaji wa seli nyekundu za damu, na mielopesisi, uzalishaji wa seli nyeupe za damu na chembe za kugandisha damu. Wakati wa utotoni, karibu kila mfupa wa binadamu huzalisha seli nyekundu za damu. Katika utu uzima, uzalishaji wa seli nyekundu za damu unafanywa na mifupa mikubwa pekee: miili ya wanyama wenye uti wa mgongo, mfupa wa kidari (sternum), ya mbavu, ya fupanyonga, na mifupa ya sehemu za juu za mikono na miguu. Tukiongezea katika kipindi cha utotoni, tezi la thaimasi, linalopatikana katika mediastinamu, ni chanzo muhimu cha limfosaiti. [13] Sehemu ya damu yenye protini (ikiwemo protini za kugandisha) huzalishwa hasa na ini, huku homoni zikizalishwa na tezi za mfumo wa mwili na sehemu ya majimaji hudhibitiwa na haipothalamasi na kudumishwa na figo.

Erithrosaiti zenye afya zina maisha ya plazma ya takribani siku 120 kabla hazijadunishwa na wengu, na seli za Kupffer katika ini. Ini pia huondoa baadhi ya protini, lipidi, na amino asidi. Figo huondoa bidhaa taka na kuzipeleka kwenye mkojo.

Usafirishaji wa oksijeni[hariri | hariri chanzo]

Pindo msingi la uloweshwaji wa himoglobini unasongezwa upande wa kulia katika hali ya kiwango cha juu cha asidi (kiwango cha juu zaidi cha dioksidi ya kaboni) na upande wa kushoto katika hali ya kiwango cha chini cha asidi (kiwango cha chini zaidi cha dioksidi ya kaboni)

Kadiri 98.5% ya oksijeni katika sampuli ya damu ya ateri katika binadamu mwenye afya anayepumua kwa kanieneo ya bahari hushikanishwa kikemikali pamoja na Hgb (Himoglobini). Kadiri 1.5% imeyeyushwa kimwili katika majimaji zingine za damu na haijaunganishwa na Hgb. Molekuli ya himoglobini ndiyo kisafirishaji kikuu cha oksijeni katika miili ya mamalia na aina nyingine nyingi (kwa wanyama wenye mfumo tofauti, angalia hapo chini). Himoglobini ina uwezo wa kuunganisha oksijeni wa kati ya 1.36 na 1.37 ml O 2 kwa gramu ya Himoglobini, [14] ambayo huongeza ujumla wa uwezo wa oksijeni ya damu mara sabini, [15] ikilinganishwa na ikiwa oksijeni pekee ingebebwa kwa umumunyifu wake wa O 0.03 mL kwa lita 2 ya damu kwa sehemu ya shinikizo ya mmHg ya oksijeni (takriban 100 mmHg katika ateri). [15]

Isipokuwa ateri za mapafu na kitovu na vena zao husika, ateri hubeba damu yenye oksijeni kutoka kwa moyo na kuipeleka kwa mwili kupitia viateri na mishipa ya damu, ambapo oksijeni hutumika; baadaye, venali, na mishipa hubeba damu isiyo na oksijeni na kuirudisha kwa moyo.

Katika hali ya kawaida kwa binadamu anayepumzika, himoglobini kwenye damu inayotoka kwenye mapafu ina ukolezo wa kama 98-99% wa oksijeni. Kwa mtu mzima mwenye afya anayepumzika, damu isiyo na oksijeni inayorudi kwenye mapafu bado ina ukolezo wa takribani 75%. [16] [17] Ongezeko la matumizi ya oksijeni wakati wa mazoezi yanayoendelea hupunguza uloweshwaji wa oksijeni kwenye damu ndani ya vena, ambayo inaweza kufikia chini ya 15% katika mwanariadha aliyepitia mafunzo; ingawa kiwango cha kupumua na mtiririko wa damu huongezeka ili kuifidia, uloweshwaji wa oksijeni kwenye damu ndani ya ateri unaweza kushuka hadi 95% au chini zaidi chini ya hali hii. [18] Uloweshwaji wa oksijeni ulio chini hivi ni hatari kwa mtu aliyepumzika (kwa mfano, wakati wa upasuaji akiwa ametiwa ganzi. Haipoksia inayoendelea (uwekaji oksijeni ulio chini ya 90%), ni hatari kwa afya, na haipoksia kali (uloweshwaji wa chini ya 30%) unaweza kusababisha kifo ghafla. [19]

Kijusi, kinachopokea oksijeni kupitia kondo, kinafikia kiwango cha chini zaidi cha shinikizo la oksijeni (kama 21% ya kiwango kinachopatikana katika mapafu ya mtu mzima), na hivyo, vijusi huzalisha aina nyingine ya himoglobini yenye mvuto wa juu zaidi kwa oksijeni (Himoglobini F ) ili kufanya kazi katika hali hii. [20]

Usafirishaji wa dioksidi ya kaboni[hariri | hariri chanzo]

Wakati damu inapotiririka kupitia mishipa, dioksidi ya kaboni huenea kutoka kwa tishu hadi kwenye damu. Kiasi kingine cha dioksidi ya kaboni huyeyushwa kwenye damu. Sehemu ya CO 2 huathiriwa na himoglobini na protini zingine na kuunda michanganyiko ya kaboni na amino. Dioksidi ya kaboni iliyobaki inabadilishwa kuwa bikaboneti na ioni za haidrojeni kupitia kitendo cha RBC cha kiondoa maji cha kaboni. Kiasi kikubwa cha dioksidi ya kaboni kinasafirishwa kupitia damu katika muundo wa ioni za bikaboneti.

Dioksidi ya kaboni (CO 2), bidhaa kuu taka kutoka kwa seli hubebwa katika damu ikiwa hasa imeyeyushwa kwenye plazma, kwa kiasi sawa na bikaboneti (HCO 3 -) na asidi ya kaboni (H 2 CO 3). 86-90% ya CO 2 katika mwili hubadilishwa kuwa asidi ya kaboni, ambayo inaweza kubadilika haraka kuwa bikaboneti, ulinganifu wa kemikali ukiwa muhimu katika ukingaji wa pH ya plazma. [21] pH ya damu huwekwa katika kadiri ndogo (pH ya kati ya 7.35 na 7.45). [9]

Usafirishaji wa ioni za haidrojeni[hariri | hariri chanzo]

Kiasi fulani cha oksihimoglobini hupoteza oksijeni na kuwa dioksihimoglobini. Dioksihimoglobini huunganisha idadi kubwa ya ioni za haidrojeni kwa kuwa ina mvuto zaidi kwa haidrojeni zaidi kuliko oksihimoglobini.

Mfumo wa limfatiki[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Mfumo wa limfu

Kwa mamalia, damu ina ulinganifu na limfatiki, ambayo huendelea kuundwa katika tishu kutoka kwa damu na kwa uchujaji wa kupita kiasi wa mshipa mdogo wa damu. Limfatiki hukusanywa kupitia mfumo wa vyombo vidogo vya limfatiki na kuelekezwa kwa mchirizi wa kifua, ambayo huielekeza katika machafu katika mshipa wa subklavia wa kushoto ambapo limfatiki huungana na mfumo wa mzunguko wa damu.

Udhibiti wa joto[hariri | hariri chanzo]

Mzunguko wa damu husafirisha joto, katika mwili na marekebisho haya ni sehemu muhimu ya udhibiti wa joto. Kuongeza mtiririko wa damu hadi kwenye sehemu ya juu (kwa mfano, wakati wa msimu wa joto au zoezi linalotumia nguvu) husababisha ngozi kupata joto, na hivyo kusababisha upoteaji wa joto kwa kasi. Kwa upande mwingine, wakati kiwango cha halijoto cha nje ni cha chini, utiririkaji wa damu kwa ncha na upande wa juu wa ngozi hupunguka na ili kuzuia joto upoteaji wa joto na husambazwa zaidi kwa viungo muhimu vya mwili.

Kazi ya Nguvumaji[hariri | hariri chanzo]

Uzuiaji wa mtiririko wa damu pia unaweza kutumika katika tishu maalum kusababisha ujazaji kwa damu unaosababisha usimikaji wa tishu hiyo, mifano ni tishu ya usimikaji katika uume na kisimi.

Mfano mwingine wa kazi ya nguvumaji ni buibui inayoruka, ambapo damu iliyolazimishwa kuelekea kwenye miguu chini ya shinikizo husababisha inyooke kwa nguvu na hivyo kuifanya iruke, bila haja ya kuwa na miguu minene yenye misuli. [22]

Wanyama wasio na uti wa mgongo[hariri | hariri chanzo]

Kati ya wadudu, damu (ambayo inaitwa vizuri zaidi hemolimfu) haihusishwi katika usafirishaji wa oksijeni (mianya inayoitwa bomba za pumzi huruhusu oksijeni kutoka kwa hewa kuenea moja kwa moja hadi kwenye tishu). Damu ya wadudu husafirisha virutubisho hadi kwenye tishu na huondoa bidhaa taka katika mfumo wazi.

Wanyama wengine wasio na uti wa mgongo hutumia protini za kupumua ili kuongeza uwezo wa kubeba oksijeni. Himoglobini ndiyo protini ya kupumua inayopatkana sana katika mazingira asili. Himosianini (buluu) ina shaba na inapatikana katika krasteshia na moluska. Inadhaniwa kwamba tuniketi (mnyama wa baharini anayetoa maji kupitia tundu mbili anapoguswa) anaweza kutumia vanabini (protini zenye vanadiamu) kwa pigmenti ya kupumua (kijani-ng'avu, buluu, au rangi ya machungwa).

Kati ya wanyama wengi wasio na uti wa mgongo, protini hizi za kubeba oksijeni huyeyuka kwa urahisi katika damu; kati ya wanyama wenye uti wa mgongo zinapatikana katika seli maalumu nyekundu za damu, zinazoruhusu ukolezi wa juu zaidi wa pigmenti za kupumua bila kuongeza mnato au kuharibu viungo vinavyochuja damu kama vile figo.

Minyoo wakubwa huwa na himoglobini zisizo za kawaida zinazowaruhusu kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida. Himoglobini hizi pia hubeba salfaidi ambazo kwa kawaida ni hatari kwa wanyama wengine.

Rangi[hariri | hariri chanzo]

Himoglobini[hariri | hariri chanzo]

Damu ya mishipa kutoka kwenye kidole kinachotoa damu
Damu ya vena iliyokusanywa wakati wa uchangaji wa damu

Himoglobini ndiyo chanzo kikuu cha rangi ya damu katika wanyama wenye uti wa mgongo. Kila molekuli ina makundi manne ya heme, na mwingiliano wao na molekuli mbalimbali hubadili rangi halisi. Kati ya wanyama wenye uti wa mgongo na viumbe vingine vinavyotumia himoglobini, damu ya ateri na damu kutoka kwa mishipa ni mwekundu wenye kung'aa, kwa kuwa oksijeni huipa kikundi cha heme rangi nyekundu iliyokoza. Damu isiyo na oksijeni huwa ni nyekundu iliyokoza zaidi; hii inapatikana katika vena, na inaweza kuonekana wakati wa uchangiaji wa damu na wakati sampuli za damu kutoka kwa vena zinapochukuliwa. Damu iliyopata yenye sumu ya monoksidi ya kaboni ni nyekundu inayoyong'aa, kwa sababu monoksidi ya kaboni husababisha uundaji wa kaboksihimoglobini. Katika sumu ya sianidi, mwili haiwezi kutumia oksijeni, kwa hivyo damu ya vena bado hubaki ikiwa na oksijeni na hivyo kuongeza wekundu. Ingawa damu yenye himoglobini kamwe haiwi na rangi ya buluu, kuna hali kadhaa na magonjwa ambapo rangi ya makundi ya heme hufanya ngozi ionekane ikiwa na rangi ya buluu. Ikiwa heme imewekewa oksijeni, methimoglobini, ambayo ni ya kahawia zaidi na haiwezi kusafirisha oksijeni, inaundwa. Katika hali isiyo ya kawaida ya salfahemoglobinemia, sehemu ya himoglobini ya ateri huwekwa oksijeni, na huonekana kuwa na rangi nyekundu iliyokoza na rangi ya bluu (sainosisi).

Vena katika ngozi huonekana kuwa na rangi ya bluu kutokana na sababu mbalimbali ambazo hutegemea rangi ya damu kwa kiwango kidogo pekee. Kujitokeza kwa sehemu nyeupe kwenye ngozi na uchakataji maono ya rangi pia huchangia. [23]

Mjusi katika kundi la Prasinohaema huwa na damu ya kijani kutokana na mkusanyiko wa bidhaa taka inayoitwa bilivedini. [24]

Himosianini[hariri | hariri chanzo]

Damu ya moluska wengi - ikiwa ni pamoja na sefalopodi na gastropodi - pamoja na baadhi ya wadudu, kama vile kaa aina ya Horseshoe, yenye rangi ya buluu, kwa kuwa ina protini za himosianini zenye ukolezi wa kama gramu 50 kwa lita. [25] Himosianini huwa haina rangi wakati haina oksijeni na ni buluu iliyokoza wakati inapoongezewa oksijeni. Damu inayozunguka ndani ya viumbe hawa, ambao kwa ujumla huishi katika mazingira baridi yenye mivuto ya chini ya oksijeni, huwa ni rangi ya kijivu-nyeupe hadi manjano hafifu, [25] na hugeuka kuwa buluu iliyokoza wakati inapoachwa wazi kwa oksijeni iliyo kwenye hewa, kama ilivyo wakati vinatoka damu. [25] Hii ni kutokana na mabadiliko ya rangi ya himosianini wakati inapoongezewa oksijeni. [25] Himosianini hubeba oksijeni katika giligili iliyo nje ya seli, ambayo ni tofauti na usafirishaji wa oksijeni ndani ya seli kwa mamalia kupitia himolobini katika RBC. [25]

Maradhi[hariri | hariri chanzo]

Matatizo makuu ya kiafya[hariri | hariri chanzo]

  • Matatizo ya kiwango
    • Jeraha linaweza kusababisha upotezaji wa damu kupitia kutoka damu. [26] Mtu mzima mwenye afya anaweza kupoteza karibu 20% ya kiasi cha damu (1 L) kabla ya dalili ya kwanza, kutotulia, kuanza, na 40% ya kiasi cha damu(2 L) kabla ya mshtuko. Thrombosaiti ni muhimu kwa ugandishaji na uundaji wa madonge ya damu, ambayo inaweza kusimamisha upotezaji wa damu. Majeraha mabaya kwa viungo vya ndani au kwa mifupa yanaweza kusababisha kutokwa na damu kwa ndani, ambayo wakati mwingine unaweza kuwa kali.
    • Kuishiwa maji mwilini kunaweza kupunguza kiasi cha damu kwa kupunguza kiwango cha katika damu. Mara nadra, hii inaweza kusababisha mshtuko (isipokuwa katika kesi kali sana) lakini huweza kusababisha kupungua kwa shinikizo la damu kunakosababishwa na kusimama na kuzirai.
  • Matatizo ya mzunguko
    • Mshtuko ni upiliziaji usio bora wa tishu, na unaweza kusababishwa na hali mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupoteza damu, maambukizi, kupunguka kwa uwezo wa moyo wa kusukuma damu.
    • Atherosklerosisi hupunguza mtiririko wa damu kupitia ateri, kwa sababu atheroma huziweka ateri kwenye mistari na kuzifanya nyembamba zaidi. Atheroma huendelea kuongezeka kulingana na umri na kuendelea kwake kunaweza kuhusishwa na sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuvuta sigara, shinikizo la damu, lipidi za ziada zinazozunguka (haipalipidemia), na kisukari.
    • Ugandaji unaweza kuunda mvilio, ambao unaweza kuzuia tezi.
    • Matatizo ya mchanganyko wa damu, kitendo cha kusukuma damu cha moyo, au wembamba wa mishipa ya damu kunaweza kuleta matokeo mengi ikiwa ni pamoja na haipoksia (ukosefu wa oksijeni) ya tishu zinazotolewa. Neno iskemia linarejelea tishu ambayo imefunikwa na damu, na infarction inarejelea kukufa kwa tishu (nekrosisi), ambako kunaweza kutokea wakati ugavi wa damu umezibwa (au ni duni sana).

Matatizo ya kihematolojia[hariri | hariri chanzo]

  • Upungufu wa damu mwilini
    • Idadi ndogo ya seli nyekundu (anemia) inaweza kusababishwa na kutoka damu, matatizo ya damu kama vile thalasemia, au ukosefu wa virutubishi, na inaweza kuhitaji kuongezewa damu. Nchi kadhaa zina benki ya damu zinazokidhi mahitaji ya damu kwa damu inayoweza kuongezewa. Mtu anayepokea damu lazima awe na aina ya damu iliyo sambamba na ile ya mtoaji damu.
    • Anemia Selimundu
  • Matatizo ya kuenea upesi kwa seli
    • Lukemia ni kikundi cha saratani za tishu zinazounda damu.
    • Uzalishaji wa seli nyingi nyekundu usiohusiana na kansa (erithremia) au uzalishaji wa chembe nyingi za kugandisha damu (thrombosaitosisi muhimu) kunaweza kusababisha kansa.
    • Dalili za Mayelodisplastiki huhusisha uzalishaji duni wa jamii ya seli moja au zaidi.
  • Matatizo ya ugandishaji
    • Himofilia ni ugonjwa wa kijenetikia unaosababisha utendakazi mbaya katika mojawapo kati ya mifumo ya ugandishaji wa damu. Hii inaweza kuruhusu majeraha ambayo kwa kawaida sio makuu yawe ya kutisha maisha, lakini kwa kawaida zaidi husababisha hemarthrosisi, au utokaji wa damu katika mianya ya maungo, ambao unaweza kusababisha ulemavu.
    • Utendakazi mbaya au idadi ndogo ya chembe za kugandisha damu pia unaweza kusababisha ugonjwa wa kugandisha (magonjwa ya kutokwa damu).
    • Hali ya kugandishwa damu (ugonjwa wa kuvilia) hutokana na kasoro katika udhibiti wa chembe za kugandisha damu au utendakazi wa kigandiza damu, na unaweza kusababisha mvilio.
  • Magonjwa ya kuambukizwa kwa damu
    • Damu ni chombo kikubwa cha maambukizi. Virusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI huambukizwa kupitia mgusano na damu, shahawa, au majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mtu aliyekwishaambukizwa. Homa ya manjano aina ya B na C husambazwa hasa kwa njia ya mgusano na damu. Kutokana na maambukizi yanayotokana na damu, vitu vilivyo na damu huchukuliwa kama bayohatari.
    • Maambukizi ya bakteria kwenye damu ni uwepobakteria au sepsisi. Kuambukizwa virusi ni viremia. Malaria na malale ni maambukizi ya damu yanayotokana na vimelea.

Usumisho wa monoksidi ya kaboni[hariri | hariri chanzo]

Dutu zingine bali na oksijeni zinaweza kuungana na himoglobini, wakati mwingine hali hii inaweza kuleta madhara yasiyoweza kubadilishwa kwa mwili. Monoksidi ya kaboni, kwa mfano, ni hatari sana inapobebwa hadi kwenye damu kupitia mapafu kwa kuvuta pumzi, kwa sababu monoksidi ya kaboni hushikana kabisa na himoglobini na kuunda himoglobini kaboksili, hivi kwamba himoglobini kidogo zaidi ina uhuru wa kuungana na oksijeni, na hivyo kiwango cha chni zaidi cha oksijeni kinaweza kusafirishwa katika damu. Hali hii huweza kusababisha kukosekana kwa hewa kwa njia fichu. Moto katika chumba kilichofungwa na kisicho na tundu za kuingiza hewa ni hatari sana, kwa kuwa kinaweza kukusanya monoksidi ya kaboni katika hewa. Kiasi fulani cha monoksidi ya kaboni huungana na himoglobini wakati wa uvutaji wa tumbaku.

Madawa ya tiba[hariri | hariri chanzo]

Bidhaa za damu[hariri | hariri chanzo]

Damu ya kuongezewa hutolewa kutoka kwa binadamu kwa uchangaji wa damu na kuhifadhiwa katika benki ya damu. Kuna aina nyingi za damu katika binadamu, mfumo wa kikundi cha damu cha ÅBO, pamoja na mfumo wa kikundi cha damu cha Rhesasi, ndiyo muhimu zaidi.

Kuongezewa damu ya kikundi kisichokubaliana na kikundi kingine cha damu kunaweza kusababisha matatizo makali, ambayo mara nyingi ni mabaya, kwa hivyo ulinganishaji mtambuko hufanywa ili kuhakikisha kuwa bidhaa ya damu iliyo sambamba inaongezewa.

Bidhaa zigine za damu zinazotolewa ndani ya vena ni chembe za kugandisha damu, plazma ya damu, krayopresipiteti, na vikolezo vya sababu maalum za kuganda.

Utoaji wa ndani ya vena[hariri | hariri chanzo]

Aina nyingi za madawa (kutoka viua vijisumu hadi tibakemo) hutolewa ndani ya vena, kwa kuwa hazifyonzwi kwa urahisi au vya kutosha na njia ya utumbo.

Baada ya upotezaji wa damu nyingi, michanganyiko iliyotegenezwa inayojulikana kama vipanua plazma vinaweza kutolewa ndani ya vena, ama michanganyiko ya chumvi (NaCl, KCl, CaCl 2 n.k ..) katika viwango vya ukolezi vya kifisiolojia, au michanganyiko ya koloidi, kama vile dekstrani, albumini ya majimaji ya damu ya binadamu, au plazma-bichi iliyoganda. Katika hali hizi za dharura, kipanuzi cha plazma ni bora zaidi kwa michakato hii ya kuokoa maisha kuliko kuongezewa damu, kwa sababu metaboli ya seli nyekundu za damu zilizoongezwa hazianzi upya mara baada ya kuongezewa.

Uondoaji wa damu[hariri | hariri chanzo]

Katika matibabu yenye misingi ya kisasa, uondoaji damu hutumika kudhibiti magonjwa yasiyo ya kawaida, ikiwa ni pamoja na hemokromatosia na kuongezeka kwa chembe nyekundu za damu. Hata hivyo, uondoaji wa damu na unyonyaji damu zilikuwa njia maarufu ambazo zilikuwa hazijahalalishwa zilizotumika hadi karne ya 19, kwa kuwa magonjwa mengi yalidhaniwa kimakosa kuwa yalitokana na kiwango cha juu cha damu, kulingana na matibabu ya Hippocrates.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tiba rasmi ya Ugiriki[hariri | hariri chanzo]

Katika tiba rasmi ya Ugiriki, damu ilihusishwa na hewa, majira ya kuchipua, na silika ya uchangamfu (sanguine). Pia iliaminika kuwa zilizalishwa na ini pekee.

Tiba ya Hipokrati[hariri | hariri chanzo]

Katika tiba ya Hipokrati, damu ilichukuliwa kama moja ya viowevu vinne, vingine vikiwa kohozi, nyongo njano, na nyongo nyeusi.

Utamaduni na imani za dini[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na umuhimu wake katika maisha, damu inahusishwa na idadi kubwa ya imani. Moja kati ya zile kuu zaidi ni matumizi ya damu kama alama ya mahusiano ya familia kupitia kuzaliwa / uzazi; kuwa na "uhusiano wa damu" ni kuhusiana kwa uzazi au nasaba, badala ya ndoa. Hii huhusiana kwa karibu na ukoo, na misemo kama vile "damu ni nzito kuliko maji", "damu mbaya" na pia "ndugu wa damu." Damu husisitizwa sana katika dini za Kiyahudi na Kikristo kwa sababu Walawi 17:11 inasema "maisha ya kiumbe yamo katika damu." Fungu hili ni sehemu ya sheria ya Kilawi inayopinga unywaji wa damu au ulaji wa nyama ambayo bado ina damu ndani yake badala ya kuimwaga nje.

Marejeleo ya hadithi kuhusu damu mara nyingine yanaweza kushikanishwa na hali ya kutoa uhai, inavyodhihirika katika matukio kama vile kujifungua, ikilinganishwa na damu ya jeraha au kifo.

Waaustralia asili[hariri | hariri chanzo]

Katika desturi za wakazi asili wa Australia, ngeu (hasa nyekundu) na damu, zote zikiwa na kiwango cha juu cha chuma na ambazo zinadhaniwa kuwa Maban (zenye nguvu za uchawi) hupakwa kwenye miili ya wachezaji wakati wa matambiko. Kama Robert Lawlor anavyosema:

Katika tamaduni na sherehe nyingi za Aborijini, ngeu nyekundu hupakwa katika sehemu zote za miili uchi za wachezaji. Katika sherehe za siri na takatifu za kiume, damu iliyoondolewa kutoka kwenye vena za mikono ya mshiriki hubadilishwa na kusuguliwa juu ya miili yao. Ngeu nyekundu pia hutumiwa kwa njia sawa na hii katika sherehe zisizo za siri. Damu pia hutumika kushikilia manyoya ya ndege kwenye miili ya watu. Manyoya ya ndege huwa na protini ambayo ina kiwango cha juu cha hisi ya magnetiki. [27]

Lawlor anasema kuwa damu inayotumika kwa njia hii inaaminika na watu hawa kuwa inawaunganisha wachezaji na dunia yenye nguvu isiyoonekana ya wakati wa ndoto. Lawlor maeneo haya yenye nguvu zisizoonekana na maeneo ya sumaku, kwa kuwa chuma ina sumaku.

Upagani katika Indo-Uropa[hariri | hariri chanzo]

Kati ya makabila ya kundi la lugha zinazohusiana na Kijerumani (kama vile Anglo-Saksoni na Normani), damu ilitumika wakati wa kutoa dhabihu zao zilizoitwa the Blóts. Damu hii ilikuwa inaaminika kuwa ina uwezo wa chanzo chake, na baada ya kuua mnyama, damu ilinyunyizwa kwenye kuta, juu ya sanamu za miungu, kwa washiriki wenyewe. Kitendo hiki cha kunyunyiza damu kiliitwa bleodsian kwa Kiingereza cha kale, na istilahi hii ilikopwa na Kanisa Katoliki na kuwa kubariki na baraka. Neno la Kihiti lenye maana ya damu, ishar lilihusiana na maneno "kiapo" na "kiunganishi":, tazama Ishara. Wagiriki wa Kale waliamini kuwa damu ya miungu, ichor, ilikuwa ni madini ambayo ilikuwa sumu kwa binadamu.

Uyahudi[hariri | hariri chanzo]

Katika Uyahudi, damu haiwezi kuliwa hata kwa kiasi kidogo (Walawi 3:17 na mahali pengine); jambo hili linajitokeza katika sheria za Kiyahudi kuhusu lishe (Kashrut). Damu huondolewa kutoka kwenye nyama kwa kuweka chumvi na kuilowesha nyama kwenye maji.

Matambiko nyingine ya damu yanahusu kufunika damu ya ndege na mawindo baada ya uchinjaji (Walawi 17:13); sababu iliyotolewa na Torati ni: "Kwa kuwa uhai wa wanyama uko ndani ya damu yake" (Walawi 17:14).

Pia ikiwa mtu wa imani halisi ya Kiyahudi amekufa kwa njia ya kinyama, sheria za kidini zinaamuru kuwa damu yake ikusanywe na izikwe pamoja na mwili.

Jambo muhimu zaidi ni kwamba kwenye Pasaka Wayahudi wanapaswa kuchinja mwanakondoo dume na kupaka milango yao kwa damu yake kama kinga. Ndivyo walivyofanya tangu kale, hasa katika Musa kuwatoa Misri.

Ukristo[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Ekaristi

Kwa Wakristo damu ya Kristo husadikiwa kuwa njia pekee ya upatanisho kwa ajili ya dhambi (1Yoh 1:7; Ufu 1:5): ndiye mwanakondoo wa kweli ambaye damu yake inawapa nguvu ya kumshinda shetani (Ufu 12:11).

Katika damu hiyo Mungu alifanya na watu agano jipya la milele, kama alivyotangaza Yesu mwenyewe katika karamu ya mwisho na mitume wake.

Baadhi ya madhehebu ya Ukristo, yakiwa ni pamoja na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Kanisa la Asiria la Mashariki hufundisha kwamba, baada ya kuwekwa wakfu, divai ya Ekaristi hubadilika na kuwa damu ya Yesu. Hivyo, katika divai takatifu, Yesu anakuwa yupo kiroho na kimwili. Mafundisho hayo yana misingi yake katika Karamu ya mwisho, kama ilivyoandikwa katika Injili nne za Biblia ya Kikristo, ambapo Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa mkate walioula ni mwili wake, na divai ni damu yake. "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu." (Luka 22:20).

Teolojia ya Walutheri hufunza kuwa mwili na damu ziko pamoja "katika, pamoja na, na chini ya" mkate na divai ya sherehe ya Ekaristi. Aina nyingine za Uprotestanti, hasa [[Wapresbiteri] na Wamethodisti, hufundisha kuwa divai ni alama tu ya damu ya Kristo, ambaye yuko kiroho lakini hayuko kimwili.

Upande wa damu ya wanyama, mitume na wazee wa Kanisa katika Mtaguso wa Yerusalemu (49 hivi) walipiga marufuku kwa Wakristo kunywa damu, pengine kwa sababu hii ilikuwa amri aliyopewa Nuhu ((Mwanzo 9:4, tazama Sheria ya Nuhu). Amri hii iliendelea kufuatwa na Waorthodoksi huko Mashariki, ingawa wataalamu wa Biblia ya Kikristo wanaonyesha kwamba katazo hilo, na mengine matatu yaliyoendana nalo, yalitolewa tu ili Wakristo wa Kiyahudi wasikwazike katika kushirikiana na Wakristo wa mataifa wasiojisikia kubanwa na masharti yote ya Torati.

Uislamu[hariri | hariri chanzo]

Ulaji wa vyakula vyenye damu ni haramu kulingana na sheria za Kiislamu kuhusu lishe. Hii inatokana na taarifa katika Kurani, Sura Al-Ma'ida (05:03): "Vilivyoharimishiwa (kama chakula) ni: nyama ya mnyama aliyefariki, damu, nyama ya nguruwe, na lolote ambalo limetajiwa juu yake jina la mwingine bali na Allah."

Damu inachukuliwa kama chafu, na katika Uislamu, usafi ni sehemu ya imani, hivyo kuna mbinu maalum za kupata hali ya usafi wa kimwili na kitambiko mara tu utokaji damu unapofanyika. Sheria maalum na amri zinahusu hedhi, kutokwa na damu baada ya kuzaa na kutokwa na damu kusio kwa kawaida kwenye uke.

Mashahidi wa Yehova[hariri | hariri chanzo]

Kulingana na tafsiri yao ya maandiko, kama vile Matendo 15:28-29 ("Endelea kujitenga ... na damu."), Mashahidi wa Yehova hawali damu wala kukubali kuongezewa damu yote au sehemu kuu za damu: seli nyekundu za damu, chembechembe nyeupe za damu, chembe za kugandisha damu (thrombositi), na plazma. Wanachama wanaweza kujiamulia binafsi ikiwa watakubali taratibu za matibabu zinazohusisha damu yao wenyewe au dutu ambazo zinagawanywa zaidi kutoka kwa sehemu nne kuu.[28]

Tamaduni za Kichina na Kijapani[hariri | hariri chanzo]

Katika tamaduni maarufu ya Uchina, mara kwa mara inasemekana kuwa, ikiwa pua la mtu limetoa kiasi kidogo cha damu, hii inamaanisha kuwa ana hamu ya ngono. Jambo hili huonekana mara nyingi katika filamu za lugha ya Kichina na Hong Kong na pia katika utamaduni wa Japani zinazotaniwa katika anime (katuni hai za sinema za Kijapani) na manga (hadithi za katuni za Kijapani zilizochapishwa). Wahusika, hasa wanaume, mara nyingi huonyeshwa wakitokwa na damu kwenye pua ikiwa wamuona mtu aliye uchi au mwenye mavazi kidogo, au kama wamekuwa na mawazo au ndoto za kiashiki; hii inatokana na dhana kwamba shinikizo la damu ya wanaume hupanda kwa kiwango kikubwa wanapopata ashiki. [29]

Kashfa za damu[hariri | hariri chanzo]

Makundi mbalimbali ya kidini na makundi mengine yamepewa shutuma za uongo kuwa yanatumia damu ya binadamu katika matambiko; shutuma hizo zinajulikana kama kashfa za damu. Aina maarufu sana ya kashfa hii ni kashfa ya damu dhidi ya Wayahudi. Ingawa hakuna tambiko inayohusisha damu ya binadamu katika sheria au desturi za Kiyahudi, uongo wa aina hii (mara nyingi unaohusiana na mauaji ya watoto) ulitumika sana katika Zama za Kati kuhalalisha mateso dhidi ya Wayahudi.

Hekaya kuhusu wanyonya damu[hariri | hariri chanzo]

Wanyonya damu ni viumbe vya visasili vinavyokunywa damu moja kwa moja ili viendelee kuishi, na hupendelea zaidi damu ya binadamu. Tamaduni kote duniani huwa na visasili vya aina hii, kwa mfano 'kisasili cha Nosferatu', binadamu anayepata kuhukumiwa na asiyekufa kwa kunywa damu ya wengine, inatokana na elimu ya mila na desturi za jamii za Ulaya Mashariki. Kupe, ruba, mbu za kike, popo zinazonyonya damu, na viumbe vingine vingi vya kiasili hunywa damu, lakini ni popo pekee anaohusishwa na wanyonya damu. Hii haina uhusiano na popo wanyonyaji damu, ambao ni viumbe vya Amerika iliogunduliwa na Wazungu baada tu ya utungaji wa visasili vya Ulaya.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Katika sayansi-tumizi[hariri | hariri chanzo]

Mabaki ya damu yanaweza kuwasaidia wapelelezi wa mahakama kutambua silaha, kuunda upya kitendo cha uhalifu, na kuwahusisha watuhumiwa na uhalifu. Kupitia uchambuzi wa sampuli ya damu, habari za mahakama pia zinaweza kupatikana kutoka kwa usambazaji wa nafasi katika sampuli za damu.

Uchambuzi wa mabaki ya damu pia ni mbinu inayotumika katika akiolojia.

Katika sanaa[hariri | hariri chanzo]

Damu ni mojawapo kati ya ugiligili wa mwili ambao umetumika katika sanaa. [30] Hasa, katika maonyesho ya mtendaji wa Viennese Hermann Nitsch, Franko B, Lennie Lee, Ron Athey, Yang Zhichao, na Kira O `Reilly, pamoja na upigaji picha wa Andres Serrano, zimehusisha damu kama kipengele kikuu cha kuona. Marc Quinn ameunda sanamu kwa kutumia damu iliyogandishwa, ikiwa ni pamoja na umbo la kichwa chake mwenyewe uliotengenezwa kwa kutumia damu yake mwenyewe.

Katika ukoo na historia ya familia[hariri | hariri chanzo]

Neno damu, hutumika katika jamii kuashiria ukoo na asili ya mtu. Maneno mengine ambapo damu hutumika katika muktadha wa historia ya familia ni damu ya buluu (kutoka tabaka la viongozi), damu ya kifalme, damu mchanganyiko (ya kutoka mbari tofauti) na jamaa wa damu (yaani ndugu).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Franklin Institute Inc.. Blood – The Human Heart. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-03-05. Iliwekwa mnamo 19 March 2009.
  2. Maton, Anthea; Jean Hopkins, Charles William McLaughlin, Susan Johnson, Maryanna Quon Warner, David LaHart, Jill D. Wright (1993). Human Biology and Health. Englewood Cliffs, New Jersey, USA: Prentice Hall. ISBN 0-13-981176-1. 
  3. Alberts, Bruce (2005). Leukocyte functions and percentage breakdown. Molecular Biology of the Cell. NCBI Bookshelf. Iliwekwa mnamo 2007-04-14.
  4. Shmukler, Michael (2004). Density of Blood. The Physics Factbook. Iliwekwa mnamo 2006-10-04.
  5. Medical Encyclopedia: RBC count. Medline Plus. Iliwekwa mnamo 18 November 2007.
  6. Robert B. Tallitsch; Martini, Frederic; Timmons, Michael J. (2006). Human anatomy (5th ed.). San Francisco: Pearson/Benjamin Cummings. p. 529. ISBN 0-8053-7211-3. 
  7. 7.0 7.1 Ganong, William F. (2003). Review of medical physiology (21 ed.). New York: Lange Medical Books/McGraw-Hill. p. 518. ISBN 0-07-121765-7. 
  8. Waugh, Anne; Grant, Allison (2007). "2". Anatomy ans Physiology in Health and Illness (Tenth ed.). Churchill Livingstone Elsevier. p. 22. ISBN 978 0 443 10102 1. 
  9. 9.0 9.1 Acid-Base Regulation and Disorders at Merck Manual of Diagnosis and Therapy Professional Edition
  10. Sellmeyer DE, Stone KL, Sebastian A, Cummings SR (January 2001). "A high ratio of dietary animal to vegetable protein increases the rate of bone loss and the risk of fracture in postmenopausal women. Study of Osteoporotic Fractures Research Group". Am. J. Clin. Nutr. 73 (1): 118–22. PMID 11124760. 
  11. Romer, Alfred Sherwood; Parsons, Thomas S. (1977). The Vertebrate Body. Philadelphia, PA: Holt-Saunders International. pp. 404–406. ISBN 0-03-910284-X. 
  12. Harvey, William (1628). Exercitatio Anatomica de Motu Cordis et Sanguinis in Animalibus (Latin).
  13. Williams, Peter W.; Gray, Henry David (1989). Gray's anatomy (37th ed.). New York: C. Livingstone. ISBN 0-443-02588-6. 
  14. Dominguez de Villota ED, Ruiz Carmona MT, Rubio JJ, de Andrés S (December 1981). "Equality of the in vivo and in vitro oxygen-binding capacity of haemoglobin in patients with severe respiratory disease". Br J Anaesth 53 (12): 1325–8. PMID 7317251. doi:10.1093/bja/53.12.1325. 
  15. 15.0 15.1 Costanzo, Linda S. (2007). Physiology. Hagerstwon, MD: Lippincott Williams & Wilkins. ISBN 0-7817-7311-3. 
  16. Upitishaji hewa safi na Utendaji wa Uvumilivu. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-03-23. Iliwekwa mnamo 2014-06-01.
  17. Msaada kuhusu upandikizaji- Mapafu, Moyo/Mapafu, Moyo Archived 24 Februari 2004 at the Wayback Machine. vikundi vya MSN
  18. Mortensen SP, Dawson EA, Yoshiga CC, et al. (July 2005). "Limitations to systemic and locomotor limb muscle oxygen delivery and uptake during maximal exercise in humans". J. Physiol. (Lond.) 566 (Pt 1): 273–85. PMC 1464731. PMID 15860533. doi:10.1113/jphysiol.2005.086025. 
  19. Mwongozo wa 'St George' kuhusu Katheta ya Ateri ya Mapafu. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-09-25. Iliwekwa mnamo 2014-06-01.
  20. [43] ^ Ubebaji wa Oksijeni katika Damu - Sehemu za juu kulingana na bahari
  21. Biology.arizona.edu. Oktoba 2006. Uwiano wa kliniki wa viwango vya pH: bikaboneti kama kinga.
  22. "Spiders: circulatory system". Encyclopedia Britannica online. http://www.britannica.com/eb/topic-559817/spider. Retrieved 2007-11-25.
  23. Kienle, Alwin; Lothar Lilge, I. Alex Vitkin, Michael S. Patterson, Brian C. Wilson, Raimund Hibst, and Rudolf Steiner (March 1, 1996). "Why do veins appear blue? A new look at an old question" (PDF). Applied Optics 35 (7): 1151–60. doi:10.1364/AO.35.001151. Archived from the original on 2012-02-10. Retrieved 2014-06-01. 
  24. Austin CC, Perkins SL (2006). "Parasites in a biodiversity hotspot: a survey of hematozoa and a molecular phylogenetic analysis of Plasmodium in New Guinea skinks". J. Parasitol. 92 (4): 770–7. PMID 16995395. doi:10.1645/GE-693R.1. 
  25. 25.0 25.1 25.2 25.3 25.4 Shuster, Carl N (2004). "Chapter 11: A blue blood: the circulatory system". In Shuster, Carl N, Jr; Barlow, Robert B; Brockmann, H. Jane. The American Horseshoe Crab. Harvard University Press. pp. 276–7. ISBN 0674011597. 
  26. Blood - The Human heart. The Franklin Institute. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-03-05. Iliwekwa mnamo 19 March 2009.
  27. Lawlor, Robert (1991). Voices of the first day: awakening in the Aboriginal dreamtime. Rochester, Vt: Inner Traditions International. pp. 102–3. ISBN 0-89281-355-5. 
  28. The Watchtower Juni 15, 2004, ukurasa wa 22, "Be Guided by the Living God" (Kuongozwa na Mungu aliye hai)
  29. Sheria ya Anime #40 kwa jina lingine Sheria ya Sanguination kwa ABCB.com , The Anime Cafe.
  30. "Nostalgia" Archived 8 Januari 2009 at the Wayback Machine. Kazi ya sanaa katika damu

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Wikimedia Commons ina media kuhusu: