Fidel Castro
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fidel Alejandro Castro Rúz (* 13 Agosti, 1926) ni kiongozi wa Kuba tangu 1959 akiwa waziri mkuu hadi 1976 halafu rais wa nchi. Baada ya upasuaji mwaka 2006 alikabidhi madaraka kwa kakaye Raul Castro.
Fidel Castro alisoma sheria kwenye chuo kikuu cha Havana akawa wakili kabla ya kujiunga na siasa ya mapinduzi.
Castro aliongoza harakati ya upinzani wa wanamgambo dhidi ya udikteta wa jenerali Fulgencio Batista tangu 1953. 1958 alishinda jeshi la Batista aliyekimbia nchi tar. 1 Januari, 1959. Castro akawa kiongozi mpya wa Kuba.
Tangu siku zile aliendelea kutawala. Castro hakukubaliwa na Marekani hivyo akajiunga na Umoja wa Kisovyeti katika siasa yake dhidi ya Marekani. Aliongoza harakati yake kuwa chama cha kikomunisti akatangaza ukomunisti mwenyewe.
Hata baada ya kuporomoka kwa ukomunisti kote duniani aliendelea kutawala.