Ujamaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Ujamaa ni dhana iliyoanzishwa kwa misingi ya sera za Julius Nyerere za maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Tanzania punde tu baada ya kupata uhuru kutoka Uingereza mwaka wa 1961. Mwaka wa 1967, Rais Nyerere alichapisha mwongozo wa maendeleo yake, ambao uliitwa Azimio la Arusha, ambapo Nyerere alionyesha haja ya mtindo wa Kiafrika wa maendeleo na huo ukawa msingi wa Usoshalisti wa Afrika. Ujamaa linatokana na neno la Kiswahili linalomaanisha familia au jamii na hujulikana kwa sifa kadhaa muhimu, yaani mtu anakuwa mtu kwa kupitia watu au jamii.


Nyerere alitumia Sheria ya kuzuia kutiwa Kizuizini kuwakamata watu kikatili kupindukia na walioathiriwa kuhesabiwa kwa maelfu. Serikali ilihamishia watu hadi mashamba ya pamoja na kuwapa ahadi ambazo baadaye ziligeuka kuwa uongo. Wengine walilazimishwa, kwa mfano, kwa kuchoma vijiji vyao. Polisi na jeshi waliojihami kwa silaha walitumika katika uhamisho wa watu [1]. Uchumi ulianguka na watu wengi walikuwa karibu kufa njaa. Taifa lilinusurika kwa kutegemea msaada ya kigeni ya chakula.


Ujamaa ulivunjwa wakati Nyerere alipomwachia mamlaka Ali Hassan Mwinyi mwaka wa 1985[2].


Yaliyomo

Ujamaa[hariri]

Nyerere alitumia Ujamaa kama msingi wa mradi wa maendeleo ya taifa. Aliitafsiri dhana ya Ujamaa kuwa mfumo wa usimamizi wa kisiasa na kiuchumi kwa namna mbalimbali:


  1. Kuweko kwa mfumo wa chama kimoja chini ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kusaidia katika kuimarisha mshikamano wa kujitegemea kwa Tanzania iliyokuwa tu imejipatia uhuru.
  2. Ustawishaji wa usawa kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kuweko kwa demokrasia kuu; kukomesha ubaguzi kwa misingi ya hali ya mtu; na kuzifanya sekta muhimu za uchumi kufikia taifa zima[3].
  3. Kupeleka uzalishaji katika vijiji, ambapo ilifanya uwezo wa uzalishaji wa aina zote kufanyika kwa pamoja.
  4. Kukuza kujitegemea kwa Tanzania kwa njia mbili: mabadiliko ya kiuchumi na mitazamo ya kitamaduni. Kiuchumi, kila mtu angekifanyia kikundi chote kazi na kujifanyia yeye mwenyewe; kitamaduni, Watanzania lazima wajifunze kujikomboa kutoka kwa utegemezi wa nchi za Ulaya. Kwake Nyerere, hii ilijumuisha Watanzania kujifunza kujifanyia mambo wao wenyewe na kujifunza kuridhika na kile ambacho wangeweza kufikia kama nchi huru.
  5. Utekelezaji wa elimu bila malipo na ya lazima kwa Watanzania wote ili kuwahamasisha wananchi kuhusu kanuni za Ujamaa[3].


Nyerere alitumia Sheria ya Kuzuia Kutiwa Nguvuni bila sababu kukandamiza vyama vya wafanyakazi na kuwakamata wapinzani kupindukia. Watu walipotea na idadi kamili haikuwahi kamwe kuchapishwa, lakini waathiriwa wanakadiriwa kuwa maelfu. Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu kama Amnesty International yalipiga kampeni dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania[4]. Vyombo vya habari vilidhibitiwa kwa kunyimwa usajili rasmi.


Nyerere aliwalazimishwa watu kuhamia kwenye mashamba ya pamoja, jambo ambalo lilitatiza shughuli za kilimo na uzalishaji. Tanzania iligeuka kutoka kuwa taifa la wakulima waliojitahidi kukidhi mahitaji yao na kuwa taifa la wakulimana walioangamia kwa njaa kwa pamoja.


Nyumba ziliteketezwa moto au kubomolewa, wakati mwingine pamoja na mali ambayo familia hizo zilikuwa nayo kabla ya Ujamaa[1]. Chakula kilipewa tu watu waliokubali kujiunga na Ujamaa[1].


Kiasi kikubwa cha utajiri wa nchi aina ya mijengo na kuboresha miundo ya ardhi (mashamba, miti ya matunda, nyua) iliharibiwa au kutelekezwa kwa lazima [1]. Mifugo waliibiwa, kupotea, kupata magonjwa, au kufa[1].


Watu waliopoteza heshima kwa tamaduni na maeneo kama vile makaburi ya mababu zao[1].


Suleman Sumra aligundua kuwa mavuno katika mashamba ya Ujamaa kwa pamoja yalikuwa chini kwa asilimia 33-85 kuliko yale ya mashamba yaliyomilikiwa kibinafsi. Kwa wastani yalikuwa chini kwa asilimia 60. Wakulima wa pamoja hawakuwa na motisha za kufanya kazi[1].


Hali ya nchi ilienea haraka na kuadhiri karibu kila sekta. Mwaka wa 1967, ustawishaji wa taifa ulibadilisha serikali na kuifanya mwajiri mkubwa zaidi katika nchi. Ilihusika katika kila kitu, kuanzia kufanya mauzo ya reja hadi biashara ya kuuza na kuagiza bidhaa kutoka ng'ambo na hata uokaji, na kuleta mazingira muafaka kwa ufisadi[5]. Ukiritimba na taratibu zisizoeleweka ziliongezeka na viwango vya juu vya kodi kuwekwa[5]. Fedha za umma zilitumika vibaya na kuweka kwa matumizi yasiyo na faida[5]. Uwezo wa kununua ulipungua kwa kiwango kikubwa mno na hata bidhaa muhimu zikawa hazipatikani[5]. Mfumo wa kutoa vibali (vibali) uliwaruhu maafisa wakuu kuchukua rushwa kubwa ili kutoa vibali[5]. Msingi wa mfumo wa ufisadi ukawa umewekwa[5].


Barabara ziliharibika na kuwa kati ya barabara mbovu zaidi Afrika. Sekta ya viwanda ikadidimia. Kampuni ya mgodi iliyomilikiwa na serikali ikaonekana kushindwa[6].


Muziki wa hip hop nchini Tanzania ulipata msukumo kutokana na mawazo na mandhari ya Ujamaa. Mwaka wa 1967, baada ya Rais Nyerere kuanzisha itikadi mpya ya kisiasa, ambayo aliahidi itawakomboa Watanzania kutoka ubeberu wa kimataifa, ilitelekezwa na wanasiasa wa Tanzania, kanuni za Ujamaa zilifufuliwa tena kupitia "njia isiyotarajiwa: Wanamuziki wa Rap na wasanii wa hip hop katika mitaa ya Tanzania[7]. Kama jawabu kwa miaka ya viongozi wafisadi wa serikali na wanasiasa baada ya Nyerere, dhana za umoja na familia na usawa zilikuwa ndio ujumbe aliotumwa katika muziki uliokuwa unatayarishwa. Hii ilikuwa kama mwitikio wa darasa la wafanya kazi katika mtazamo fulani ilikuwa upinzani. [8]Kanuni za uchumi wa ushirika -"wananchi wa kawaida kushirikiana ili kujipatia mahitaji muhimu ya maisha" - [9] ni maneno yanayoweza kuonekana katika nyimbo nyingi za hip hop za wasanii wa Tanzania. Zinapigia upatu ukuzaji wa biashara na kujitegemea katika jitihada za kuinua mioyo za vijana na kuhamasisha mabadiliko katika jamii.


Benki ya Dunia imekosolewa kwa kuchangia mpango huo: "Nchini Tanzania, kwa mfano, Benki hii ilitoa fedha kwa kampeni ya udikteta wa Julius Nyerere unaoitwa Ujamaa, ni mfano wa mfumo wa vijiji wa Mengistu. Wakulima walipoteza uhuru wao, na nchi ilichukua ardhi yao na kudai mazao yao, yote haya kwa msaada na baraka za Benki ya Dunia. Katika miaka michache tu, Nyerere aligeuza nchi yake kuwa gofu, taifa la waombaji. Lakini Benki hii haijawahi kukubali makosa haya[10].


Tazama Pia[hariri]


Marejeo[hariri]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 Challenging nature: local knowledge, agroscience, and food security in Tanga. Philip Wayland Porter. 
  2. David Edward O'Connor. The basics of economics, 100. 
  3. 3.0 3.1 Pratt, Cranford (1999). "Julius Nyerere: Reflections on the Legacy of his Socialism". Canadian Journal of African Studies 33 (1): 137 – 52. doi:10.2307/486390. 
  4. Colin Legum, G. R. V. Mmari. Mwalimu: the influence of Nyerere. 
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 Rick Stapenhurst, Sahr John Kpundeh. Curbing corruption: toward a model for building national integrity, 153–156. 
  6. [24] ^ [https: / / www.policyarchive.org/bitstream/handle/10207/9616/89356_1.pdf?sequence=1 Tanzania's travail: Lessons in improving American aid to the Third World]
  7. Lemelle, Sidney J. "'Ni Wapi tunakwenda': Hip Hop Culture and the Children of Arusha. " In the Vinyl Ain't Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
  8. Lemelle, Sidney J. "'Ni Wapi tunakwenda': Hip Hop Culture and the Children of Arusha. " In The Vinyl Ain't Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
  9. [27] ^ Denied: 1up!Software
  10. Deressa, Yonas. Subsidizing tragedy: The World Bank and the new colonialism.


Viungo vya nje[hariri]