Ali Hassan Mwinyi
| Ali Hassan Mwinyi | |
|
|
|
| Muda wa Utawala 5 November 1985 – 23 November 1995 |
|
| Waziri Mkuu | Joseph Sinde Warioba |
|---|---|
| mtangulizi | Julius Nyerere |
| aliyemfuata | Benjamin Mkapa |
|
|
|
| tarehe ya kuzaliwa | 8 Mei 1925 Zanzibar |
| utaifa | Mtanzania |
| chama | |
| ndoa | Siti Mwinyi |
| dini | Uislamu |
Ali Hassan Mwinyi (amezaliwa 8 Mei 1925) alikuwa Rais wa Pili wa Tanzania kuanzia 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Kabla hajachaguliwa kuwa Rais, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Rais. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia 1990 hadi 1996.
Mwinyi alizaliwa kwenye kisiwa cha Unguja (Zanzibar).
Wakati wa urais wa Mwinyi, sera za Ujamaa zilianza kugeuzwa. Badala yake sera za soko huru zilianzishwa, masharti ya kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje yalipunguzwa na uanzishaji wa biashara ya watu binafsi ulihamasishwa. Mwaka wa 1991, uanzishaji wa vyama vingi uliruhusiwa.
Sera za soko huru za Mwinyi zimeendelezwa chini ya Rais Benjamin Mkapa. Mwinyi mwenyewe, baada ya kustaafu, hakujiingiza katika mambo ya siasa tena. Anaendelea kuishi huko Dar es Salaam.
| Alitanguliwa na Mwinyi Aboud Jumbe |
Makamu wa Rais wa Tanzania 1984-1985 |
Akafuatiwa na Joseph Sinde Warioba |
| Alitanguliwa na Julius Nyerere |
Rais wa Tanzania 1985-1995 |
Akafuatiwa na Benjamin Mkapa |
| Orodha ya Marais wa Tanzania | |
| Julius Nyerere • Ali Hassan Mwinyi • Benjamin Mkapa • Jakaya Kikwete |