Thabo Mbeki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Thabo Mbeki
Thabo Mbeki

Thabo Mvuyelwa Mbeki (amezaliwa 18 Juni, 1942) ni Rais wa nchi ya Afrika Kusini tangu 14 Juni, 1999. Alimfuata Nelson Mandela.

Mbeki alilelewa katika familia ya Waxhosa katika jimbo la Rasi Mashariki. Wazazi walikuwa walimu wa shule na wanachama wa ANC.

[hariri] Mwanaharakati wa ANC

Thabo alishiriki katika shughuli za chama hiki wakati alipokuwa mwanafunzi. Baada ya kukamatwa kwa Nelson Mandelea na viongozi wengine wa ANC alitoka nchini akapelekwa Uingereza aliposoma elimu ya uchumi kwenye chuo kikuu cha Sussex. Baada ya masomo akajiunga na utumishi wa ANC na tangu 1971 alichaguliwa katika kamati kuu akawa mwakilishi wa ANC katika nchi mbalimbali za Afrika.

Tangu 1989 Mbeki alikuwa katibu wa chama mambo ya nje akahudhuria katika majadilioano kati ya serikali ya Afrika Kusini na ANC kuhusu namna za kumaliza sera ya Apartheid.

[hariri] Makamu wa Rais na Rais

Baada ya uchaguzi huru wa kwanza nchini Afrika Kusini mwaka 1994 alikuwa makamu wa rais chini ya Nelson Mandela. Mwaka 1997 akawa mwenyekiti wa ANC badala ya Mandela. 16 Juni 1999 akaapishwa kama rais wa Afrika Kusini akarudishwa katika uchagizi wa Aprili 2004.

Katika Desemba 2007 Mbeki aligombea tena nafasi ya mwenyekiti wa ANC lakini alishindwa na Jacob Zuma.


[hariri] Viungo vya Nje

BBC kuhusu Thabo Mbeki

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Thabo Mbeki" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Thabo Mbeki kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Vifaa binafsi