Shelisheli
|
|
|||
| Wito: Finis Coronat Opus. (Kilatini "Matokeo ni taji la kazi") |
|||
| Lugha rasmi | Seselwa, Kiingereza, Kifaransa | ||
| Mji Mkuu | Victoria | ||
| Serikali | Jamhuri | ||
| Rais | James Alix Michel (tangu tar. 14 Aprili 2004) | ||
| Eneo | 455 km² | ||
| Idadi ya wakazi | 80.832 (Julai 2004) | ||
| Wakazi kwa km² | 177 | ||
| Uhuru | 29 Juni 1976 (kutoka Uingereza) | ||
| Pesa | Rupia ya Shelisheli | ||
| Wakati | UTC +4 | ||
| Wimbo la taifa | Koste Seselwa | ||
![]() |
|||
Shelisheli ni funguvisiwa na jamhuri katika Bahari Hindi mbele ya mwambao wa mashariki ya Afrika upande wa kaskazini wa Madagaska.
Yaliyomo |
Jiografia [hariri]
Shelisheli ina visiwa 115; 32 kati ya hivyo ni visiwa vikubwa kidogo vyenye milima, vingine ni vidogo na huitwa "Visiwa vya nje".
Kisiwa kikubwa zaidi ni Mahé na mji mkuu Victoria uko huko. Wakazi wengi huishi Mahe pamoja na visiwa vya karibu, hasa Praslin na La Digue.
Visiwa hivyo vina milima inayofikia hadi 900 m juu ya UB. Mkubwa ni Morne Seychellois wenye mita 905 juu ya UB. Hali ya hewa ni ya kitropiki ikiwa halijoto iko kati ya 24 °C na 30 °C. Kiasi cha mvua ni kati ya 2.880 mm (huko Mji Mkuu Victoria na 3.550 mm mlimani.
Wakazi [hariri]
Wakazi kwa jumla ni machotara wenye mchanganyiko wa damu ya Ulaya, Afrika bara na Madagaska. Licha ya hao kuna vikundi vidogo vya Wazungu, Wachina na Wahindi halisi. Walio wengi (90%) ni Wakristo Wakatoliki, idadi ndogo ni Waprotestanti, wengine wachache ni Wahindu, Wabudha au Waislamu.
Historia [hariri]
Hakuna hakika kuhusu wakazi wa kwanza. Inaaminika ya kwamba ndio mabaharia na wafanyabiashara Waarabu. Taarifa ya kwanza imepatikana kutoka kwa Wareno waliozunguka hapa kuanzia mwaka 1505.
Kwa karne moja na nusu meli au jahazi zilipitia Shelisheli tu kwa kusudi la kuchota maji ya kunywa au kukusanya matunda bila ya kuanzisha makao ya kudumu. Majambazi wa baharini walipenda kujificha Shelisheli.
Ndio Ufaransa iliyojenga vituo vya kwanza vya kudumu mwaka 1756. Wafaransa waliita visiva "Seychelles" kwa heshima ya waziri wa Kifaransa wa siku zile Jean Moreau de Sechelles.
Walowezi wao walianzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara wakitumia watumwa kutoka Madagaska na Afrika bara kwa ajili ya kazi yenyewe. Tangu mwaka 1814 visiwa vilikuwa chini ya Uingereza. Waingereza walivumilia walowezi na utamaduni wa Kifaransa visiwani.
Kwanza Shelisheli zilikuwa zikitawaliwa pamoja na Mauritius, lakini mwaka 1903 visiwa vilipewa cheo cha koloni mbali na Mauritius. Mwaka 1970 Shelisheli walipata uhuru. Katiba ya kwanza ilifuata mfano wa Uíngerezeza lakini mwaka 1979 katiba mpya ilileta mfumo wa chama kimoja. Tangu 1993 katiba ilisahihishwa tena ikiruhusu vyama vingi vya kisiasa.
Chama kilichopata kura nyingi ndicho SPPF (Seychelles People's Progressive Front).
Uchumi [hariri]
Biashara ya Shelisheli ni hasa utalii. Asilimia 30 hivi za wafanyakazi wote wamo katika utalii. Biashara hii inaingiza 70% ya pato la taifa.
Pamoja na utalii, uvuvi na kilimo ni muhimu pia.
Viungo vya nje [hariri]
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Shelisheli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Nchi za Afrika | |
|---|---|
| Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
| Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
| Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia | |
