Gabon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Gabon (Kiswahili)
Bendera ya Gabon Nembo ya Gabon
(Bendera ya Gabon) (Nembo ya Gabon)
Lugha rasmi Kifaransa
Mji Mkuu Libreville
Mji Mkubwa Libreville
Serikali Jamhuri
Kaimu Rais Brice Clotaire Oligui Nguema
Eneo km² 267,668
Idadi ya wakazi 2,397,368 (2023)
Wakazi kwa km² 7.9
Uchumi nominal Bilioni $17.2
Uchumi kwa kipimo cha umma $8,384
Pesa CFA frank (XFA) (Frank ya Afrika ya Kati)
Kaulimbiu "Uungano, Kazi, Haki"
Wimbo wa Taifa Concord
Gabon katika Afrika
Saa za Eneo UTC +1
Mtandao .ga
Kodi ya Simu +241

Jamhuri ya Gabon (kifupi: Gabon) ni nchi huru ya Afrika magharibi ya kati.

Imepakana na Guinea ya Ikweta, Kamerun, Jamhuri ya Kongo na Ghuba ya Guinea.

Nchi hii ina umma mdogo, madini na mali kwa wingi, na wafanyabiashara kutoka nchi za kigeni wameweza kufanya Gabon iwe nchi yenye maendeleo makubwa.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya Gabon.

Maeneo ya utawala[hariri | hariri chanzo]

Gabon imegawiwa katika mikoa 9 nayo ina jumla ya wilaya (départements) 37.

Mikoa ni:

Historia[hariri | hariri chanzo]

Aliyekuwa Rais Omar Bongo Ondimba wa Gabon (kushoto) akiwa Washington, USA.

Jamhuri ya Gabon, tangu kupata uhuru kutoka Ufaransa tarehe 17 Agosti 1960, imeongozwa na Rais watatu, Léon M'ba, El Hadj Omar Bongo ambaye amekuwa kiongozi kutoka mwaka wa 1967 hadi kifo chake (2009: ndiye aliyekuwa kiongozi barani Afrika aliyeshikilia uongozi kwa muda mrefu zaidi), halafu mwanae Ali aliyepinduliwa na wanajeshi tarehe 30 Agosti 2023.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Nyumba ya baraza, Libreville

Mwaka wa 1990 Gabon ilianza demokrasia ya vyama vingi na katiba ya kidemokrasia ili ruhusu ukweli wa uchaguzi na uwajibikaji wa idara za serikali, lakini hali iliendelea kuwa karibu ileile.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Gabon ni nchi yenye neema sana kuliko nchi jirani. Uchumi wake, hasa chumo cha umma, ni mara nne ya nchi za Afrika kusini kwa Sahara. Hii hasa ni kwa sababu ya uzalishaji wa mafuta ambao umeleta utajiri na mali, lakini usambazaji wa mali hii ya mafuta bado umedhoofika.

Gabon ilikuwa mwanachama wa Muungano wa Nchi Zinazouza Mafuta (OPEC) kutoka mwaka wa 1975 mbaka 1995.

Mwaka 1990, udhaifu wa pesa CFA frank uliacha Gabon katika shida ya kulipa deni za kimataifa; Ufaransa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wameipa Gabon mkopo na usaidizi kwa uelewano kwamba Gabon itageuza uchumi wake barabara.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Yasemekana mambo ya mazingira yalifanya umma wa Gabon kutopanda kwa sensa kati ya miaka 1900 na 1940.

Ni nchi ambayo ina umma mdogo zaidi katika Afrika bara, na upungufu wa wafanyakazi ni mojawapo ya mambo yanayofanya hasa uchumi kutovuma zaidi.

Umma hasa kwa ujumla ni kama watu milioni 2.4.

Gabon hasa ina makabila zaidi ya 40 ambayo yana utamaduni na lugha tofauti lakini karibu wote (95%) ni wa jamii ya Bantu. Wafang ndio kabila kubwa zaidi nchini Gabon, wengine ni Wamyene, Wabandjabi, Waeshira, Wabapounou na Waokande.

Lugha ya Kifaransa ndiyo lugha rasmi ya taifa ambayo hutumika kwa mawasiliano (wakazi wanaoimudu ni 80%). Wafaransa 10,000 wanaishi Gabon, na Ufaransa unaathiri mambo ya kigeni, utamaduni na biashara nchini Gabon.

Upande wa dini, imekadiriwa kwamba 75.6% za wakazi ni Wakristo (hasa Wakatoliki), 12.2% ni Waislamu (hasa wageni), na 5.7% wanafuata dini asilia za Kiafrika (Bwiti).

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • David E. Gardinier and Douglas A. Yates, Historia elekezo ya Gabon, tolezi ya 3. (The Scarecrow Press, Inc., 2006)
  • David E. Gardinier, Kamusi ya Historia ya Gabon, tolezi ya 2. (The Scarecrow Press, Inc., 1994) – kazi inayohusu maelezo biografia ya vifaa 1,453
  • James F. Barnes, Gabon: Beyond the Colonial Legacy (Boulder: Westview, 1992)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Serikali[hariri | hariri chanzo]

Habari[hariri | hariri chanzo]

Uchambuzi[hariri | hariri chanzo]

Koo na makabila[hariri | hariri chanzo]

Maelekezo[hariri | hariri chanzo]

Utalii[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Gabon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.