Cabo Verde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Cabo Verde (Kiswahili)
Repúblika di Kabu Verdi (Krioli)
Bendera ya Cabo Verde Nembo ya Cabo Verde
(Bendera ya Cabo Verde) (Nembo ya Cabo Verde)
Lugha rasmi Kireno
Mji Mkuu Praia
Mji Mkubwa Praia
Serikali Jamhuri
Rais José Maria Neves
Waziri Mkuu Ulisses Correia e Silva
Eneo km² 4,033
Idadi ya wakazi 483,628 (2021)
Wakazi kwa km² 123.7
Uchumi nominal $ Bilioni 2.042
Pesa Eskudo ya Cabo Verde
Kaulimbiu "Umoja, Kazi, Maendeleo"
Wimbo wa Taifa Chimbo ya Uhuru
Cabo Verde katika Afrika.
Ramani ya Cabo Verde.

Cabo Verde (kwa Kiing. Cape Verde) ni nchi ya visiwa katika bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika ya Magharibi.

Umbali wake na Senegal ni km 460.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Eneo la visiwa vyake kwa jumla ni km² 4,033.

Funguvisiwa lake lina visiwa 15 katika vikundi viwili:

Miji[hariri | hariri chanzo]

Mji mkuu ni Praia katika kisiwa cha Santiago.

Miji mikubwa zaidi ni (takwimu za mwaka 2010): Praia (wakazi 127,832), Mindelo (wakazi 70,468), Santa Maria (wakazi 23,839), Assomada (wakazi 12,026), Pedra Badejo (wakazi 9,345) na São Filipe (wakazi 8,125).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Hadi kufika kwa Wareno katika karne ya 15 visiwa vya Cabo Verde havikuwa na watu.

Wareno walianzisha mashamba ya miwa na kuleta watumwa kutoka bara la Afrika.

Cabo Verde ilikuwa pia kituo muhimu cha biashara ya watumwa kati ya Afrika na Amerika.

Wahamiaji kutoka Ulaya walikuwa pia Wahispania, Waitalia pamoja na Wayahudi na Waislamu waliokataliwa kukaa kwao Ureno.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na historia hiyo, leo idadi kubwa ya wakazi ni machotara waliozaliwa na Waafrika (waliochangia 56% ya DNA) na Wazungu (waliochangia 44%).

Lugha rasmi ni Kireno, lakini wakazi wanazungumza zaidi aina mbalimbali za Krioli iliyotokana na lugha hiyo.

Upande wa dini, walau 89.1% ya wakazi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (78.7%), lakini pia wa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (10.4%).

Kutokana na hali ngumu ya uchumi, wananchi wanaoishi nje ya Cabo Verde ni mara mbili kuliko wale wanaoishi nchini. Kati ya waliohama baada ya uhuru (1975), 500,000 wanaishi Marekani na 150,000 Ureno. Hata hivyo kuna wahamiaji vilevile, hasa kutoka nchi za Afrika bara.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Cabo Verde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.