Morisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Morisi


Ramani ya kisiwa cha Morisi

Morisi ni kisiwa karibu na Afrika, pia ni nchi inayoitwa rasmi Jamhuri ya Morisi (kwa Kiingereza: Republic of Mauritius, kwa Kifaransa: République de Maurice). Ni nchi ya visiwa katika Bahari Hindi takriban Km 900 mashariki kwa Madagaska na km 4000 kusini-magharibi kwa Bara Hindi.

Nchi ilipata uhuru tarehe 12 Machi 1968, ikawa jamhuri tarehe hiyohiyo mwaka 1992.

Eneo la jamhuri ni pamoja na kisiwa cha Morisi yenyewe, kisiwa cha Rodrigues, visiwa vidogo vya Cargados Carajos na Agalega.

Hivyo vyote ni sehemu ya funguvisiwa la Maskarena pamoja na kisiwa cha Kifaransa cha Réunion.

Mji mkuu wa jamhuri ni Port Louis.

Eneo la Jamhuri ya Morisi[hariri | hariri chanzo]

Visiwa vya jamhuri vimesambaa katika eneo pana sana:

Kisiwa kikuu cha Mauritius ni km² 1,865 au 91% za ardhi yote ya jamhuri. Karibu wakazi wote (1,261,208) huishi huko.

Kisiwa cha Rodrigues kipo km 560 mashariki kwa Morisi yenyewe. Eneo lake ni km² 109; kuna wakazi 41,000.

Visiwa vya Makarena kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi

Visiwa vya Cargados Carajos (vinaitwa pia Saint Brandon) ni visiwa 16 vidogo sana, vyenye eneo la km² 1.3 pekee. Viko km 300 kaskazini kwa Morisi. Kuna wakazi mia chache wavuvi.

Agalega ni visiwa viwili, yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini, takriban km 1,122 kaskazini kwa Morisi yenyewe. Visiwa hivyo vina eneo la km² 70. Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa cha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini. Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga kwa matumizi yao wenyewe.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Watu wa Morisi ni mchanganyiko mkubwa kutokana na historia ya visiwa hivyo.

Baada ya Waarabu na Wareno kuvumbua Morisi, wakazi wa kwanza (1638) walikuwa Waholanzi, lakini hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.

Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi, Wafaransa walipeleka pia watumwa kutoka bara la Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000, pia Wahindi 587.

Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon. Tangu siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali, lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja za Kifaransa.

Baada ya kuwapatia watumwa uhuru, Waingereza walileta Wahindi wengi, baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Kihindi.

Lakini 80% ya wananchi hutumia aina ya Kifaransa kama lugha ya kwanza (pamoja na krioli ya Kimorisyen. Asilimia 15 hutumia lugha za Kihindi kama vile Kibhojpuri, Kiurdu, Kitamil, na wengine Kichina na Kiingereza.

Karibu nusu (48.5%) ya wakazi hufuata dini ya Uhindu, 32.7% Ukristo (hasa wa Kanisa Katoliki), 17.3% ni Waislamu (hasa Wasunni, lakini pia Washia), 0.4% Wabuddha.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Hadi leo kilimo cha miwa (sukari) ni uti wa mgongo wa uchumi wa Morisi.

Nchi iliendelea kuwa na serikali zilizochaguliwa bila kupinduliwa: hali hii ya utulivu ilisaidia kukua kwa uchumi. Hali ya maisha ni ya juu kuliko nchi nyingi za Afrika.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Morisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.