Praia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Praia
Nchi Cabo Verde
Praia inavyoonekana kutoka ndege.

Praia ni mji mkuu wa jamhuri ya Cabo Verde iko kisiwani Santiago.

Praia ikiwa na wakazi 159,000 hivi (2017) ni mji mkubwa kabisa pamoja na kuwa kitovu cha uchumi cha nchi.

Biasharanje inayopitia katika bandari ya Praia ni hasa kahawa, miwa na matunda.

Kuna uwanja wa ndege wa kimataifa.