Omar Bongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Omar Bongo

Amekufa 2009
aliaga dunia nchini morrocco
Nchi Gabon
Majina mengine bongo ondiba
Cheo Rais

|thumb|right|Omar Bongo]] El Hadj Omar Bongo Ondimba (30 Desemba 19358 Juni 2009) alikuwa Rais wa nchi ya Gabon tangu mwaka wa 1967. Baadhi ya marais barani Afrika, Bongo ameshika urais kwa muda mrefu kabisa. Alimfuata Leon M'ba akiwa na umri wa miaka 31 tu, na wakati ule alikuwa rais kijana kabisa duniani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Albert-Bernard Bongo. Kiongozi huyo mwanzoni alitambulika kama Albert Benard Bongo kabla ya baadae kusilimu na kuitwa Omari Bongo. baada ya kumaliza masomo yake ya awali na sekondari mjini Brazzaville, Bongo alianza kazi katika shirika la umma lililokuwa likishughulika na masuala ya posta na simu lakini baadae aliingia kwenye mafunzo ya kijeshi na taratibu ukawa mwanzo wa kujikita kwenye siasa.

Kiongozi huyo amevunja rekodi ya kuwa Rais aliyekaa muda mrefu marakani kuliko Rais yeyote barani Afrika. Rais huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73, ambapo ameiongoza Gabon kwa miaka 42. Bongo alijiunga na serikali ya Gabon mwaka 1965 na mwaka 1967 akawa makamu wa Rais ambapo mwaka huo huo akashika hatamu ya kuwa Rais wa nchi hiyo kufuatia cha kifo cha ghafla cha Rais Leon Mba. Bongo alipoingia madarakani alijenga utawala imara ambao ulinufaika zaidi baada ya kugunduliwa kwa mafuta nchini Gabon ingawa utajiri wake ulinufaisha idadi ndogo ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni 1.5. kitu kilicholeta lawama kubwa kwa kiongozi huyo. Rais huyo amefariki dunia wakati akipata tiba ya saratani jijini Barcelona nchini Hispania. Rais Bongo ameaga dunia takribani miezi mitatu baada ya kifo cha mkewe, Edith Lucie Bongo Ondimba (45) aliyefariki dunia 14 Machi mwaka huu wakati akipata tiba mjini Rabat nchini Morocco. Bongo na Edith walifunga ndoa mwaka 1990. Edith aliuguzwa kwa miezi kadhaa nchini Morocco, na umma haukutangaziwa sababu za kifo chake. Edith alikuwa binti wa Rais wa Congo, Denis Sassou Nguessou. Mwanaharakati huyo wa mapambano dhidi ya Ukimwi alikuwa mke wa pili kwa Bongo, mke wa kwanza wa Rais huyo alikuwa, Josephine Nkama.

Habari za kifo cha Rais huyo wa Gabon zilikuja wiki chache baada ya mahakama nchini Ufaransa kutaka kufanyiwa uchunguzi juu ya mali ya Rais Bongo nchini Ufaranasa. Uchunguzi kama huo pia utafanyiwa mali ya rais wa Kongo Brazzaville Dennis Sassou Nguesso na rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang` Nguema. Shirika la kupambana na rushwa Transparency International, tawi la Ufaransa linawalaumu viongozi hao kwa kutumia fedha za umma, kununua nyumba katika nchi za nje na pia kwa kununua magari ya kifahari, madai ambayo viongozi hao wameyakanusha. Ripoti iliyotolewa na serikali ya Gabon ilisema kuwa, ilithibitisha kuwa rais Bongo alikuwa amelazwa katika zahanati moja nchini Uhispania lakini haikutaja chochote kuhusiana na maradhi ya saratani, baada ya madai kuwa rais Bongo alikuwa akiugua saratani ya utumbo. Pia ripoti hiyo ilisema kuwa kiongozi huyo hajafanyiwa upasuaji wowote na kuvilaumu vyombo vya habari kwa kueneza uvumi wenye lengo la kuivuruga Gabon.

Akiwa ziarani nchini Cameroon waziri mkuu wa Ufaransa Francois Fillon alisema kuwa rais Bongo alikuwa katika hali nzuri hadi kufikia mapema hapo jana. Mnamo tarehe sita mwezi huu rais Bongo anayeitawala Gabon kwa miaka arobaini na moja sasa, alisema kuwa angesitisha kwa muda shughuli zake ili kupumzika na pia kuomboleza kifo cha mkewe aliyeaga dunia mwezi machi mwaka huu. Mkewe Edith Lucie Bongo ambaye ni mtoto wa rais wa kongo Brazzaville Denis Sassou Ngueso, aliaga dunia nchini morrocco akiwa na umri wa miaka arobaini na tano, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Habari kutoka afisi ya rais zilisema kuwa, rais Bongo alipatwa na mshutuko baada ya kifo cha mkewe.

Pia jeshe baada ya miaka 56 ya nchi hiyo kuongozwa na familia ya bongo ondiba ambaye aliongoza nchi hiyo kama Rais kuanzia mwaka 1967 hadi 2009 nakisha mwanae Ali bongo akamrithi na kuongoza Nchi hiyo hadi uchaguzi mkuu wa August 2023 ambako pia alitangazwa Mshindi na kuendelea kusalia madarakani.