Tuvalu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Tuvalu
Bendera ya Tuvalu Nembo ya Tuvalu
Bendera Nembo
Wito la taifa: Tuvalu mo te Atua
(Kituvalu ya "Tuvalu kwa ajili ya Mola")
Wimbo wa taifa: Tuvalu mo te Atua
Lokeshen ya Tuvalu
Mji mkuu
Vaiaku (kijiji),
Fongafale (kisiwa), Funafuti (atolli)
8°31′ S 179°13′ E
Mji mkubwa nchini --
Lugha rasmi Kituvalu, Kiingereza
Serikali Ufalme wa kikatiba
Elizabeth II wa Uingereza
Filoimea Telito
Apisai Ielemia
Independence
kutoka Uingereza

1 Oktoba 1978
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
26 km² (ya 227)
(kidogo sana)
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
10,441 (ya 222)
441/km² (ya 22)
Fedha Dollar ya Tuvalu
Dollar ya Australia (AUD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+12)
(UTC)
Intaneti TLD .tv
Kodi ya simu +688

-


Tuvalu ni nchi ya visiwani ya Polynesia katika Bahari ya Pasifiki kati ya Hawaii na Australia. Nchi jirani katika bahari ni Kiribati, Samoa na Fiji.

Jina la Tuvalu lamaanisha "visiwa nane" kwa sababu kiasili ilikuwa na visiwa 8 vilivyokaliwa na watu. Kisiwa cha tisa kimepata wakazi tangu 1943.

Ramani ya Tuvalu

Eneo[hariri | hariri chanzo]

Eneo lake ni visiwa vinne na atolli tano jumla eneo la 26 km². Kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa Tuvalu ni cnhi yenye wakazi wachache kabisa.

Tuvalu ina visiwa na atolli vifuatavyo:

Nchi itakayopotea karibuni[hariri | hariri chanzo]

Kama nchi mbalimbali za visiwani Tuvalu iko hatarini ya kupotea katika miaka 50 inayokuja. Kimo cha juu cha visiwa vyake ni mita 5 pekee juu ya UB. Kubadilika kwa hali ya hewa duniani na kupanda kwa uwiano wa bahari kutamaanisha ya kwamba sehemu kubwa sana la eneo lake litazama polepole chini ya maji.

Serikali imeshaomba majirani wakubwa kama Australia na New Zealand kuwapokea wenyeji wake. New Zealand imekubali na kwa sasa kila mwaka watu 74 wanahamia New Zealand ambayo ni tayari kuwapokea pia wengine itakapokuwa lazima. Kuna mipango ya kuwapa makazi ya pamoja kwa kusidi ya kuhifadhi utamaduni wao.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tuvalu imekaliwa na watu wa Polynesia ikawekwa chini ya usimamizi wa Uingereza katika karne ya 19 kwa jina la "Ellis Islands". Kati ya 1892 hadi 1916 ilikuwa eneo lindwa na baadaye sehemu ya koloni ya Gilbert and Ellice Islands hadi 1974. Mwaka ule wenyeji walipigia kura pendekezo la kuwa pekee na visiwa vya Gilbert vilivyokuwa Kiribati baadaye. Tuvalu ikapata uhuru wake 1978.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tuvalu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | New Zealand | Niue | Pitcairn | Polynesia ya Kifaransa | Palau | Papua New Guinea | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna