Pitcairn

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hori la Bounty kwenye Pitcairn; nyumba za Adamstown zaonekana upande wa kulia juu
Ramani ya visiwa

Pitcairn ni kisiwa katika Pasifiki na pia jina la kundi la visiwa ambalo ni eneo la ng'ambo la Uingereza la pekee katika Pasifiki. Visiwa vingine havina wakazi.

Mji mkuu ni kijiji cha pekee cha Adamstown.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Pitcairn ni kisiwa chenye asili ya kivolkeno. Eneo lake ni 4.6 km² na idadi ya wakazi ni 46. Visiwa vingine ni atolli za Oeno, Henderson na Ducie. Watu walio karibu wako kwenye kisiwa cha Pasaka (2,000 km) na kwenye Polynesia ya Kifaransa (500 km).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Hakuna uhakika kuhusu wakazi na wageni wa Pitvcairn kabla ya kugunduliwa na kijana Pitcairn kwenye jahazi ya Kiingereza mwaka 1767. Inaaminiwa ya kwamba Wapolynesia walikalia visiwa tangu karne kadhaa lakini hakuna uhakika kama walikuwepo bado wakati wa kufika kwa Wahispania waliopita sehemu hizi katika karne ya 17. Waingereza hawakukuta tena watu.

Tangu 1790 kisiwa kilikaliwa na waasi wa Bounty iliyokuwa jahazi ya Kiingereza ambako uasi wa mabaharia dhidi ya nahodha. Waasi waliamua kujificha kwa sababu waliogopa hukumu ya mauti kulingana na sheria za uingereza za wakati ule. Wakazunguka bahari pamoja na wanawake wa Tahiti wakakuta Pitcairn wakajenga makazi yao kisiwani.

1838 kisiwa kilitangazwa kuwa koloni ya Uingereza.

Mwaka 1856 watu wa Pitcairn walihamishwa Kisiwa cha Norfolk kwa sababu walikuwa wengi mno kulingana na udogo wa kisiwa wakaona njaa. Lakini familia tano waliamua kurudi tena na wale ni mababu wa wakazi wa leo.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi unategemea hasa kilimo cha kijungujiko na misaada kutoka Uingereza. Mara chache kisiwa kinatembelewa na watalii.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | New Zealand | Niue | Pitcairn | Polynesia ya Kifaransa | Palau | Papua New Guinea | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna